TANGAZO
Na Clarence Chilumba,
Masasi.
Chumba cha kuhifadhia
magodoro pamoja na vifaa vingine katika shule ya sekondari ya bweni ya
wasichana ya Ndwika iliyopo kata ya Lulindi Halmashauri ya wilaya ya Masasi
mkoani Mtwara kimeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa katika shule
hiyo.
Vifaa vilivyoteketea katika
tukio hilo ni magodoro 225 pamoja vifaa vingine vya wanafunzi hao ikiwemo
mashuka,sare za shule,nguo za michezo,chandarua,madaftari pamoja na vyombo vya
kulia chakula ikiwa ni baadhi tu ya vifaa ambavyo vilivyohifadhiwa kwenye chumba hicho baada ya shule hiyo
kufungwa.
Aidha thamani ya hasara ya
moto huo inakadiriwa kufikia shilingi milioni saba kwa magodoro pekee huku
vifaa vingine vikiwa bado thamani yake haikuweza kupatikana mara moja huku
jitihada za kufanya tathimini zikiendelea.
Tukio hilo limetokea leo
majira ya saa 4:00 kamili asubuhi katika chumba cha stoo hiyo ambacho pia hutumika
kama zahanati na kwamba chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme ambapo katika
tukio hilo hakuna mtu yeyote aliyepoteza maisha au kujeruhiwa.
Chumba kilichoteketea kwa moto huo |
Mabaki ya magodoro hayo
Baadhi ya wanafunzi wakiwa na majonzi wasijue cha kufanya
Mkuu wa shule akitoa maelezo mbele ya katibu tawala
Mabaki ya chumba hicho
Mwanafunzi akipita juu ya mabaki ya magodoro
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD