TANGAZO
Mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi ambaye pia ni naibu waziri wa TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Kassimu Majaliwa
Na Clarence Chilumba,Ruangwa.
Mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi ambaye pia ni
naibu waziri wa TAMISEMI anayeshughulikia elimu Kasimu Majaliwa amewataka
madiwani pamoja na watendaji wa Halmashauri hiyo kusimamia ukusanyaji mapato ya
ndani ya Halmashauri hiyo ili waweze kutekeleza miradi ya maendeleo iliyopo
wilayani humo.
Aidha majaliwa ametoa angalizo kwa baadhi ya watendaji
wa halmashauri hiyo wenye tabia ya kutengeneza vitabu vya risiti vya kwao
kuacha mara moja kwani kwa kufanya hivyo kutaikosesha halmashauri mapato.
Pia amewataka madiwani kutoa ushirikiano kwa watendaji
wa Halmashauri hiyo katika zoezi la ukusanyaji wa mapato na kwamba kwa
kuwaachia watendaji peke yao ni kukwepa majukumu yao waliyopewa na wananchi
waliowachagua.
Hayo aliyasema leo wakati anaongea na madiwani pamoja
na watendaji wa halmashauri hiyo kwenye kikao cha kupitia na hatimaye kupitisha
bajeti ya Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi kwa mwaka wa fedha wa
2015/2016 kwenye ukumbi wa Rutesco wilayani Ruangwa.
MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA WAKIFUATILIA MKUTANO WA BARAZA HILO
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA REUBEN MFUNE AKISISITIZA JAMBO
MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA AMBAYE PIA NI DIWANI WA KATA YA MITOPE ISSA LIBABA WAKATI ANAONGEA NA MADIWANI PAMOJA NA WATENDAJI(HAWAKO PICHANI)
MAKAMU MWEYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYAYA RUANGWA AMBAYE PIA NI DIWANI WA KATA YA NAMBILANJE MOSA MTEJELA WAKATI ANATOA KILIO CHAKE KUHUSU BARABARA
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD