TANGAZO
Na Clarence Chilumba,
Masasi.
Mkazi wa kijiji cha
Nakachindu kata ya Mkundi Halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani hapa Asumini
Bakiri (39) amefikishwa kortini kujibu shitaka la mauaji linalomkabili la
kumuua mume wake aliyetambuliwa kwa jina la Simoni Simoni (45).
Mtuhumiwa huyo
alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo jana na kusomewa shitaka lake na
mwendesha mashtaka Iddi Shabani mbele ya hakimu wa mahakama ya wilaya ya Masasi
Halfani Ulaya.
Alidai kuwa mshtakiwa
huyo alitenda kosa hilo Januari 1 mwaka huu huko katika kijiji cha Nakachindu
wilayani Masasi majira ya saa 1:00 usiku ambapo mtuhumiwa alimuua mumewe kwa
kile kinachodaiwa kuwa ni sumu mara baada ya kutokea kwa ugomvi kati yao.
Iddi alidai kuwa siku ya
tukio marehemu alinunua upupu unaoliwa pamoja na nyama ya mbuzi nusu kilo kwa
ajili ya sherehe ya mwaka mpya lakini katika hali ya kushangaza usiku ulipofika
marehemu alihitaji chakula lakini mke wake alidai kuwa hakuna unga na kwamba
angeenda jirani kuomba.
Akiwa ametoka nyumbani
kwenda jirani kuomba unga huo marehemu alianza kula ile nyama na baada ya
kumaliza alianza kutokwa na povu jeupe kinywani mithili ya mtu aiyepewa sumu
huku hizo nyama zikiwa zimekwama shingoni mwake.
Mkewe alipofika alimkuta
mumewe akiwa tayari ameshapoteza fahamu na kwamba alifariki dunia akiwa kwenye
pikipiki alipokuwa akipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu na kwamba
uchunguzi wa awali unaonesha kuwa marehemu aliwekewa sumu kwenye nyama hiyo.
Hata hivyo mshtakiwa
hakuweza kupata dhamana na kurudishwa rumande ambapo kesi hiyo imehairishwa
hadi januari 19 mwaka huu itakapotajwa tena.
Katika hatua nyingine
Godfrey Clemence (26) mkazi wa kijiji cha Lukuledi wilayani Masasi jana
amefikishwa mahakamani hapo kujibu shitaka la kumuua Hamisi Abdallah (27)
ambaye pia ni mkazi wa Lukuledi kwa sababu ya wivu wa kimapenzi.
Mtuhumiwa huyo alitenda
kosa hilo mnamo Januari 1 mwaka huu majira ya saa 7:00 usiku huko katika kijiji
cha Lukuledi kesi hiyo imehairishwa na itatajwa tena januari 19 mwaka huu na
mtuhumiwa anaendelea kusota rumande.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD