TANGAZO
Na Clarence Chilumba, Masasi.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ahmadi Mwembe (37) mkazi
wa mkuti Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara amepandishwa kwa mara ya
kwanza kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Masasi kujibu shitaka
linalomkabili la kubaka.
Mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa
shitaka na mwendesha mashtaka koplo Suleimani Omari mbele ya hakimu mfawidhi Halfani
Ulaya.
Omari alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa la kubaka januari
13 mwaka huu saa 9:00 jioni huko katika mtaa wa Kisiwani kata ya Mkuti
Halmashauri ya mji wa Masasi ambapo alimbaka mtoto mwenye umri wa miaka 14
(jina linahifadhiwa) akiwa chooni nyumbani kwao.
Alidai kuwa mtuhumiwa huyo alifanikiwa kufanya kitendo hicho
cha kinyama chooni nyumbani kwao mtoto huyo ambapo siku ya tukio wazazi wa
mtoto huyo hawakuwepo nyumbani hapo kwa kuwa walielekea hospitali ya misheni ya
Ndanda kwa ajili ya kuona wagonjwa.
Omari aliieleza mahakama kuwa mshtakiwa alipewa kazi ya
ujenzi wa banda la nyumba kwa wazazi wa mtoto huyo na kwamba alitumia mwanya
huo kumrubuni mtoto huyo ili atimize ndoto zake zilizopelekea kumsababishia
maumivu makali mtoto huyo.
Maelezo ya awali kutoka jeshi la polisi wilayani hapa
yanaonesha kuwa mshtakiwa alikiri kosa la kumbaka mtoto huyo kwa madai kuwa eti
ni mpenzi wake wa muda mrefu na kwamba hadi sasa kwa nyakati tofauti imefanya
nae mapenzi mara tatu.
Alisema kuwa harakati za kumtongoza mtoto huyo alizianza
tangia mwishoni mwa Desemba mwaka jana na kwamba alidai kuwa alimkubalia awe
mpenzi wake licha ya kukiri kuwa kwa wakati huo hakuwahi kufanya nae mapenzi
kutokana na mazingira ya nyumbani kwao mtoto huyo kuwa magumu.
“Ni kweli nimefanya mapenzi na mtoto huyu nyumbani kwao
chooni siku hiyo jioni kwa kuwa wazazi wake hawakuwepo ila huyu ni mpenzi wangu
na hii ni mara yangu ya tatu kufanya nae mapenzi”.Alisema mshtakiwa huyo.
Lakini katika hali ya kushangaza mtuhumiwa huyo
alipopandishwa kizimbani jana mahakamani hapo na kutakiwa kutoa maelezo yake
alikana kutenda kosa hilo na kwamba hamjui mtoto huyo hata jina lake halijui
anachofahamu yeye ni kuwa alikuwa anafanya kazi ya kujenga nyumba nyumbani kwa
mzazi wa mtoto huyo Twalibu Katuya.
Mwendesha mashtaka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo
haujakamilika hivyo aliiomba mahakama kuahirisha shauri hilo hadi pale
upelelezi utakapokamilika.
Hakimu alihairisha kesi hiyo hadi januari 30, 2015 na
mtuhumiwa huyo kurudishwa rumande mara baada ya kushindwa kutimiza masharti ya
dhamana yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili watakaoweka bond ya shilingi milioni
kumi kila mmoja.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD