TANGAZO
Na Haika Kimaro, Lindi.
Wazazi wasiokuwa na uwezo wameshauriwa kutafuta njia mbadala
ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu badala ya kuwaacha bila
msaada wowote mazingira yanayopelekea kujiingiza katika vitendo viovu.
Wito huo umetolewa na Katibu Mtendaji wa shirika lisilo la
kiserikali la Community Health Issues and Development Association (CHIDA)
Alfred felician wakati anazungumza na
wanafunzi waliomaliza darasa la saba mwaka 2014 ambpo alisema wana changamoto
kubwa ya kupata ada jambo linalokwamisha wao kuendelea na elimu ya sekondari.
Felician alisema kutokana na uwezo mdogo wa shirika wamekuwa
wakilipia ada wanafunzi 20 ambao wako sekondari na kuiasa jamii kutofumbia
macho suala la elimu kwa watoto wao.
Alisema kuwa shirika hilo limekuwa na utamaduni wa kufanya
tathmini kwa kila mwaka ili kubaini watoto wanaoishi katika mazingira magumu
ambao wamefaulu lakini wamekosa ada hivyo kuwachukua na kufanya mazungumzo na
Halmashauri ya mji wa Lindi ambapo husaidia watoto hao kuendelea na elimu ya
sekondari.
Hata hivyo aliongeza kuwa kumekuwa na tabia ya wazazi kukaa
bila kutoa taarifa kwenye vyombo husika pale wanaposhindwa kulipa ada za watoto
wao na kuwataka kutokuwa na kificho juu ya tatizo hilo.
Felician alisema kuwa shirika lina mpango wa kufungua kituo
cha mawasiliano (information center) kwa ajili ya kujifunza kutumia mtandao ili
kujisomea na iwe sehemu ya watoto, vijana na wanawake kupata taarifa mbalimbali
ikiwemo kutafuta masoko ya biashara kwa akina mama wajasiliamali walioko katika
vikundi mbalimbali.
“Kweli watoto wanahaki ya kupata elimu wanahaki ya kusoma
lakini wanakosa ada vipato vya wazazi wao havikidhi mahitaji ya familia jambo
linalofanya mzazi ashindwe kulipa ada ya mtoto, ada ikipatikana mahitaji mengine
inakuwa ni mtihani kwao, jamii na wadau waone umuhimu wa kuwasidia”.Alisema
Felician.
Mwisho
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD