Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

CHAMA CHA MAOFISA MAWASILIANO SERIKALINI (TAGCO) CHATOA MSAADA HOSPITALI YA LIGULA-MTWARA.

TANGAZO
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO Assah Mwambene (kulia) akikabidhi kwa niaba ya Maafisa Mawasiliano Serikalini msaada wa Kitanda cha wagonjwa kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Ligula Mkoani Mtwara Dkt. Mohamed Abraham Gwao walipotembelea Hospitalini hapo.

Na Clarence Chilumba, Mtwara.
Chama cha maofisa mawasiliano serikalini (TAGCO) wametoa msaada wa vifaa katika hospitali ya mkoa wa Mtwara Ligula vitakavyotumika katika hospitali hiyo ili kupunguza tatizo la vifaa linaloikabaili hospitali hiyo.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na kitanda kimoja kitakachotumika na wagonjwa mara baada ya kufanyiwa upasuaji pamoja na mashine moja ya upasuaji (Sunction Machine) vifaa ambavyo thamani yake haikuweza kupatikana mara moja.

Akikabidhi msaada huo kwa mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya Ligula mkoani Mtwara mkurugenzi wa idara ya Habari  maelezo Assay Mwambene alisema chama cha maofisa mawasiliano waliguswa na tatizo la vifaa lililokuwa linaikabili hospitali hiyo.

Alisema msaada huo ni kwa ajili na wananchi wanaohudumiwa katika hospitali hiyo na kwamba ni vyema vifaa hivyo vikatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kusaidia jamii na Mtwara na nchi jirani ya Msumbiji  ambao kwa kiasi kikubwa hutegemea kupata huduma kwenye hospitali ya mkoa.

Kwa mujibu wa Mwambene alisema kuwa chama cha maofisa mawasiliano serikalini ni wadau wa maendeleo hapa nchini hivyo kwa kutoa msaada huo kwa hospitali ya mkoa wa Mtwara ni kama ufunguo na kwamba hakusita kuwaomba wadau wangine wa ndani na nje ya nchi kuweza kujitokeza kuisaidia hospitali hiyo.
Akipokea msaada huo mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Mtwara Dkt. Mohamedi Gwao alisema msaada huo umefika wakati muafaka na kwamba kwa kipindi kirefu watu mbalimbali wamekuwa wakijitokeza kutoa misaada tofauti na huo uliotolewa na Tagco ambao kwa kiasi kikubwa ni suluhisho la vifaa kwenye chumba cha upasuaji.

Alisema wamefurahishwa na moyo wa upendo walionao chama hicho katika kujali matatizo yanayowakabili wananchi na kwamba waendeleea kuisaidia hospitali hiyo ya mkoa pale wanapokuwa na msaada wowote ule.

Mwisho. 


 Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO Assah Mwambene (kulia) akikabidhi kwa niaba ya Maafisa Mawasiliano Serikalini msaada wa sanction mashine kwa muwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula Mkoani Mtwara Dkt. Mohamed Abraham Gwao walipotembelea Hospitalini hapo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Innocent Mungy.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  Sihaba Nkinga akitembelea katika eneo la mradi wa nyumba za wafanyakazi wa Mradi wa kuchakata Gesi Tanzania Mnazi Bay and Songo Songo Gas Processing Plant  wakati wa ziara ya Maafisa Mawasiliano Serikalini  Mkoani Mtwara. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari – MAELEZO  Zamaradi Kawawa na Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Nishati na Madini  Badra Masoud(katikati).

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  Sihaba Nkinga(katikati) akitembelea katika katika eneo la Mradi wa kuchakata Gesi wa Tanzania Mnazi Bay and Songo Songo Gas Processing Plant wakati wa ziara ya Maafisa Mawasilano Serikalini katika eneo la mradi huo katika eneo la Madimba Mkoani Mtwara

 Mhandisi Jane wa TPDC akielezea jambo kwa Maafisa Mawasiliano Serikalini  walipofanya ziara ya kutembelea Mradi wa Kuchakata Gesi wa Tanzania Mnazi Bay  and Songo Songo Gas Processing Plant uliopo katika kijiji cha Madimba Mkoani Mtwara. Watatu kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  Sihaba Nkinga. 

Pichani ni Bomba ambalo litatumika kusafirisha Gesi kutoka Mtwara hadi Kinyerezi jijini Dar es Salaam.

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top