TANGAZO
DC MASASI AWACHARUKIA WAFUGAJI MAPARAWE
Na Clarence Chilumba,
Masasi
Mkuu wa Wilaya ya Masasi Farida Mgomi amewapa siku saba
wafugaji wa jamii ya wamang’ati waliopo katika kijiji cha maparawe kata ya
sindano Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kuondoka baada ya kuvamia
mashamba ya wakulima na kuharibu mazao pamoja na ardhi yao.
Alitoa kauli jana
wakati wa mkutano mkuu wa kijiji hicho uliokuwa
na lengo la kujadili hatima ya wafugaji
hao kwa kuwa wamekuwa wakisababisha hasara ya mazao yao pamoja na kuharibu ardhi yao wanayoitegemea kwa kilimo.
Aidha wananchi hao waliojawa na hasira walitoa tamko lao
mbele ya mkuu huyo wa wilaya kuwa hawapendi wafugaji hao katika kijiji chao
kwani katika mpango wao wa ardhi hawana
eneo kwa ajili ya wafugaji wanaotoka nje
ya kijiji hicho na kwamba walichofanya wafugaji hao ni uvamizi utakaoleta
mgogoro.
Alisema wanakijiji hao wanapaswa kuwa wavumilivu kwa kipindi
chote kufuatia ukaidi waliouonesha wafugaji hao kwani hata walipoambiwa
waondoke hawakutii amri hiyo na kwamba uvuilivu wao umesaidia kuwepo kwa amani
na usalama kijijini hapo.
“Mimi kama msimamizi wa maendeleo, ninawapa siku saba muwe
tayari mmeshaondoka pamoja na mifugo yenu… na kwamba mnatakiwa kuondoka kwa kwa
amani na usalama na endepo mtakaidi
agizo hili nguvu itatumika kuwaondoa”.Alisema.
Mgomi alisema kutokana na wafugaji hao kuvamia kijijini hapo
huenda msimu wa mwaka huu ukawa wa shida kwa wakazi wa maeneo hayo kutokana na
mazao yao kuharibiwa na mifugo hiyo.
Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya Masasi Dunford
Peter alisema kutokana na sheria ya ardhi ya mwaka 1999 serikali ya kijiji ina
wajibu wa kupanga na kusimamia matumizi
ya ardhi na kwamba kwa kuwa wana kijiji hao wamekosa eneo la kutosha kwa ajili ya
wafugaji ni vyema wakaondoka.
“Hiki tunachokifanya kwenu si ubaguzi ila tumefuata sheria
kwani kijiji ndicho chenye mamlaka ya kukubali au kukataa matumizi ya ardhi kwa
shughuli yoyote inayotaka kufanyika katika kijiji chao”. Alisema.
Naye mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi
Beatrice Dominic alisema ni busara wafugaji hao wakaondoka na kwamba kwa
kuendelea kubaki bila ridhaa ya wanakijiji hao hakutakuwa na amani na usalama n
kwamba watakosa ushirikiano.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD