TANGAZO
MIKOPO YAFAIDISHA WANAWAKE MASASI
Na Clarence
Chilumba, Masasi.
Vikundi 11 vya
wanawake wajasiliamali vilivyopo Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara
vilivyopewa mkopo wa fedha shilingi milioni saba kutoka mfuko wa Taifa wa
maendeleo ya wanawake wenye lengo la kuboresha maisha ya wanawake hapa nchini
vimeanza kunufaika na mikopo hiyo.
Aidha baadhi ya vikundi
hivyo hadi sasa vimeweza kuanzisha shughuli mbalimbali za uzalishaji mali
ikiwemo utengenezaji wa batiki, makapu, kofia, vitambaa, pamoja na mazulia ya
majumbani mazingira yatakayosaidia wanawake hao kujiondoa kwenye wimbi la
umaskini.
Pia baadhi ya vikundi
hivyo vimekuwa vikijihusisha na shughuli za kilimo,biashara pamoja na ufugaji
wa kuku na kanga ili waweze kupata fedha za marejesho ili vikundi vingine vya
wanawake kama wao viweze kupatiwa fedha hizo ili nao waweze kunufaika kupitia
mikopo hiyo yenye riba nafuu.
Hayo yalibainika wakati
wa ziara maalumu jana ya ukaguzi wa vikundi hivyo uliofanywa na maofisa kutoka
idara ya maendeleo na ustawi na jamii Halmashauri ya mji wa Masasi iliyokuwa na
lengo la kujionea bidhaa zinazozalishwa na vikundi hivyo.
Akizungumza mara baada
ya ziara hiyo Kaimu ofisa ustawi wa jamii Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani
humo Pendo Malimilo alisema vikundi vingi kati ya hivyo 11 vilivyopewa mikopo
vimeweza kufikia malengo na mikakati iliyojiwekea ikiwemo ya kupambana na
umaskini.
Alisema baadhi ya
vikundi bado vinaonekana kusuasua katika utekelezaji wa yale mambo ya msingi
waliyokubaliana nao hivyo endapo vitaendelea na utaratibu huo basi
havitaingizwa kwenye orodha ya awamu ya pili ya mikopo hiyo kwa kuwa vitakuwa
vimeshindwa kutimiza viogezo na masharti ya mikopo hiyo.
Malimilo alisema katika
ukaguzi huo wamebaini mapungufu kadhaa kwenye vikundi hivyo ambayo ni lazima
wayatafutie ufumbuzi kwa lengo la kuwasaidia akinamama hao.
Moja ya vikundi
vilivyotembelewa katika ziara hiyo ni pamoja na kikundi cha chama cha wajane
Masasi (Chawamasi) ambacho hadi sasa kimeweza kupata faida iliyopo benki kiasi
cha shilingi milioni 3 na kwamba shughuli kubwa wanazozifanya ni ufumaji wa vitambaa,
kofia pamoja na mazulia.
Katibu wa kikundi hicho
cha Chawamasi Monika Chigogoro alisema licha ya mafanikio hayo bado
wanakabiliwa ni changamoto kubwa ya maneno ya kashfa na kejeli kutoka kwa
akinamama wenzao kuwa wanachama wa kikundi hicho wengi wao ni wale wanaoishi na
virusi vya Ukimwi kutokana na waume zao kufariki dunia.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD