TANGAZO
WANUSURIKA KIFO AJALINI
Na Clarence Chilumba,
Masasi.
Abiria zaidi ya 20
wamenusurika kifo kufuatia gari waliyokuwa wakisafiria Toyota Hiace kutoka
Mangaka wilayani Nanyumbu kuja Masasi mkoani Mtwara kuigonga kwa nyuma Bajaj na
hatimaye kuacha njia kwenye eneo la makutano ya barabara ya Mtwara-Masasi.
Ajali hiyo imetokea
jana majira ya saa 6:00 mchana ambapo gari lenye namba za usajili T 843 BVW
Toyota Hiace lililokuwa likiendeshwa na dereva Juma Mzee (55) mkazi wa Masasi
kuigonga kwa nyuma Bajaj yenye namba T 351 CMT ikiendeshwa na Alouter William
(36) mkazi wa Masasi.
Mkuu wa polisi wilaya
ya Masasi mkoani hapa Ndagile Makubi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kusema kuwa ajali hiyo ilitokea jana majira saa 6:00
mchana katika eneo la makutano ya barabara itokayo Mtwara kuja Masasi ambapo
gari hiyo iliigonga kwa nyuma Bajaj iliyokuwa inajaribu kuvuka kuelekea upande
wa pili.
Alisema gari hiyo lililokuwa na abiria zaidi ya 20 lilikuwa likitokea Mangaka wilayani
Nanyumbu kuja mjini Masasi na kwamba lilipofika katika eneo la makutano
ya barabara karibu na ofisi za
Tanesco liliigonga kwa nyuma Bajaj na
kuburutwa kuelekea eneo la Skaba.
Makubi alisema abiria wote pamoja na dereva
waliokuwa kwenye gari hiyo hakuna aliyejeruhiwa na kwamba dereva wa Bajaj
alipata michubuko kidogo begani ambapo alitibiwa katika Hospitali ya Mkomaindo
na hali yake inaendelea vizuri.
Katika hatua nyingine
gari ndogo lenye namba za usajili T 445 CMF Toyota Cresta lililokuwa
likiendeshwa na Christopher Gama (26) mkazi wa mtaa wa Maendeleo liliigonga ubavuni
Bajaj yenye namba za usajili T 628 CGA likiendeshwa na Hamis Athumani (21)
mkazi wa mtaa wa mkuti.
Katika ajali hiyo
hakuna aliyejeruhiwa na kwamba chanzo cha ajali hizo zote ni uzembe na kukosa
umakini kwa madereva wa vyombo hivyo vya moto.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD