TANGAZO
MASASI WAKAMILISHA MAABARA ASILIMIA
81
Halmashauri
ya mji wa Masasi mkoani Mtwara imekamilisha
ujenzi wa maabara katika shule zake za sekondari zilizopo kwenye halmashauri
hiyo kwa asilimia 81 ili kutekeleza agizo la Raisi lililozitaka shule zote za
sekondari za serikali hapa nchini kuwa na maabara tatu.
Pia
Halmashauri hiyo kwa kutumia vyanzo vyake vya mapato vya ndani tayari
imeshapeleka fedha shilingi milioni 15 kwa shule ambazo hazijamaliza ujenzi huo
wa maabara lengo likiwa ni kukamilisha ujenzi huo mwishoni mwa Desemba 25 mwaka
huu.
Akizungumza
jana na waandishi wa habari wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya ukaguzi
wa ujenzi wa maabara kaimu mkurugenzi wa
Halmashauri ya mji wa Masasi Henry Kagogoro alisema Halmashauri hiyo imejipanga
kutekeleza agizo la Raisi kwa asilimia 100 mwishoni mwa desemba mwaka huu.
Alisema
kati ya vyumba 27 vya maabara vinavyohitajika ni vyumba vitano pekee ndivyo
ambavyo hadi sasa ujenzi wake unaendelea na kwamba vingi kati ya hivyo viko
kwenye hatua nzuri ya umaliziaji huku vyumba vingine vikiwa katika hatua ya
upandishaji wa kuta zake.
Alisema
miongoni mwa shule tisa za sekondari zilizopo ndani ya Halmashauri hiyo saba
tayari zimekamilisha huku mbili zikiendelea na ujezni huo na kwamba baadhi ya
vyumba vya maabara hizo zimeshaanza kutumika huku zingine zikisubiri vifaa pamoja
na samani.
Kagogoro
alisisitiza kuwa ili kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo kwa wakati amepanga
ratiba maalumu ya kila siku kwa wakuu wa idara na vitengo ambao wanatakiwa
kufuatilia hali halisi ya ujenzi wa maabara hizo badala ya kusubiri taarifa
wakiwa ofisini.
Kwa
mujibu wa kaimu mkurugenzi huyo alisema kuwa hali ya ujenzi wa maabara katika
Halmashauri hiyo ni nzuri huku akitoa wito kwa wakuu wa shule,bodi za shule
pamoja na jamii kwa ujumla waunge mkono jitihada zinazofanywa na halmashauri
katika kuhakikisha kuwa kila shule inakuwa na maabara za masomo ya sayansi.
“Kimsingi
wanahabari, hatua tuliyofikia kwa sasa ni nzuri ingawa bado tunayo kazi kubwa
ya kufanya katika hili…tumejipanga kikamilifu na kwamba tutahakikisha kuwa
tunakamilisha ujenzi wa maabara zetu ili kutekeleza agizo la Raisi wa Jamhuri
ya muungano wa Tanzania”.Alisema.
Alisema mikakati iliyopo ni kuimarisha
miundombinu katika maabara hizo ikiwemo maji, kemikali pamoja na vifaa vingine
muhimu vinavyotumika katika maabara kwa lengo la kuwajengea uwezo na ufaulu wa
masomo ya sayansi wanafunzi wa shule hizo.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD