Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

#Maofisa Mawasiliano Wa Serikali Nchini Watakiwa Kufanya Kazi Kimkakati Katika Utoaji Wa Taarifa Kwa Wananchi.

TANGAZO
 Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China Zhao Qizheng na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Hassan Abbas wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini, leo Jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wakimsikiliza Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China, Zhao Qizheng, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini, Leo Jijini Dar es Salaam


Maafisa Mawasiliano Serikalini wametakiwa kufanya kazi zao kimkakati ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao hasa kwenye kipindi hiki cha Awamu ya Tano.

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara na Taasisi za Serikali Waziri wa zamani wa Habari wa Jamhuri ya watu wa China, Mhe. Zhao Qizheng amesema ni muhimu kwa Serikali kuhakikisha kuwa mawasiliano yote yanalenga kuwainua wananchi wake.

“Msemaji wa Serikali inabidi uwe makini katika kazi zako kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati”, alisema Qizheng.

Akifafanua Mhe. Qizheng amesema kuwa ili Tanzania Iweze kufikia maendeleo ya kweli ni muhimu kujenga mfumo dhabiti wa Mawasiliano ya Serikali kwa Umma.

Katika kutekeleza majukumu yao Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini kama wasemaji ni lazima wawe na uelewa mpana kuhusu masuala yanayohusu sekta wanazosimamia ili kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa wananchi.

Pia aliwataka Wasemaji wa Serikikali kujiandaa kabla ya kujibu hoja mbalimbali za kitaifa na Kimataifa zinazohusu Serikali na wananchi ili kutoa taarifa sahihi kwa Vyombo vya habari.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Hassan Abbas amesema ni dhamira ya Serikali kuwasiliana kimkakati ili kuchochea maendeleo.

“Lengo letu ni Kuhakikisha kuwa tunafanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa mawasiliano ya Serikali na wananchi ili kuwapa fursa ya kutoa mrejesho”alisema Abbas.

Katika kuhakikisha azma hiyo inatumia Abbas amebainisha kuwa kwa sasa Serikali inajipanga kufanya maboresho ya mifumo ya Mawasiliano ya Serikali.

Aidha Mawasiliano ya Serikali katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya Tano yanalenga kubadilisha maisha ya wananchi kutoka hali duni kwenda kwenye hali bora.

Mkutano kati ya Waziri wa Zamani wa Habari wa China na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara na Taasisis za Serikali umelenga kujenga uwezo wa Wasemaji wa Serikali ili waweze kuwasiliana na Wananchi kimkakati.


TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top