Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

#Moto Wateketeza Baadhi Ya Vyumba Vya Madarasa Shule Kongwe Ya Sekondari Lindi.

TANGAZO


Vyumba Tisa vya madarasa vimeteketea katika shule ya sekondari ya Lindi, kufuatia kuzuka kwa moto mkubwa ulioanza kuwaka majira ya saa Saba za usiku kutokana na hitilafu kwenye mfumo wa umeme.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi Renata Mzinga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa, mbali na vyumba hivyo, athari zingine zilizotokana na moto huo ni kuteketeza matundu 26 ya vyoo, ofisi 4 za walimu pamoja na vyumba viwili vya maabara za Kemia na Fizikia.

“Ulianzia kwenye ‘Main switch’..chumba ambacho kina ‘Main Switch’ kwa mujibu wa mtoa taarifa za awali ambaye ni mwalimu wa shule hiyo na kwa sababu pale shuleni hakuna namna ya kuingiza zima moto
Na Kusema……

Miundombinu ilizuia kuingiza gari la zima moto kwa hiyo wananchi wakawa wanajitahidi kuuzima kwa kuchota maji hiyo ikapelekea moto kusambaa..”alisema Kamanda.

Aidha, alisema hakuna madhara mengine yoyote yaliyojitokeza dhidi ya binadamu na kwamba bado wanafunzi walikuwa hawajaanza kuwasili shuleni hapo kutoka makwao walikokuwa kwa likizo.



TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top