Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

#Mfanyabishara Atakayeshindwa Kulipia Leseni Ya Biashara Ndani Ya Mji Wa Masasi Kufungiwa Biashara Yake...

TANGAZO
Ofisa Biashara wa Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara Masoud Mwinjuma (kulia) akimwamuru kufunga Banda la Biashara yake mmoja wa wafanyabiashara ya Salon katika eneo la Nyasa Magengeni  kwa kosa la kuendesha Biashara hiyo pasipo kuwa na Kibali au Leseni.

TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI.
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI ANAWAKUMBUSHA WAFANYABIASHARA WOTE KUWA NA LESENI HAI ZA BIASHARA.

LESENI ZA BIASHARA KWA MWAKA MPYA WA SERIKALI 2016/2017 ZITAANZA KUTOLEWA KESHO TAREHE 1/07/2017 NA KWAMBA WALE WOTE WATAKAOSHINDWA KULIPA NDANI YA SIKU 21 WATATOZWA FAINI.

KUMBUKA KUENDESHA BIASHARA BILA KUWA NA LESENI HAI NI KINYUME NA SHERIA YA LESENI ZA BIASHARA NA.25 YA MWAKA 1972 NA.3 (1, 2 & 3).

MFANYABIASHARA YEYOTE ATAKAYEBAINIKA KUFANYA BIASHARA KINYUME NA SHERIA HII ATACHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA KAMA ILIVYOAINISHWA KATIKA KIFUNGU NA.10 (1) & (2).

MWISHO WAFANYABIASHARA WOTE WANASISITIZWA KUFUATA MASHARTI YA LESENI,IKIWA NI PAMOJA NA KUWEKA LESENI ZAO SEHEMU ZA WAZI KATIKA MAENEO YAO YA BIASHARA KWANI KUTOFANYA HIVYO NI KWENDA KINYUME NA MATAKWA YA SHERIA YA LESENI KIFUNGU NA. 14 (1).

Clarence Chilumba,
Ofisa Habari Halmashauri ya Mji wa Masasi
30/06/2016.

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top