Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

#Mkuu Wa Mkoa Wa Mtwara Kuwaongoza Wananchi wa Mji Wa Masasi Kufanya Usafi #JULAI 30,2016.

TANGAZO

MKUU WA MKOA WA MTWARA KUWAONGOZA WANA MASASI SIKU YA USAFI JULAI 30, 2016.
Siku ya usafi wa mazingira hufanyika kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kote nchini ambapo kwa upande wa Halmashauri ya mji wa Masasi usafi utafanyika kimkoa siku ya tarehe 30/7/2016 kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 10:00 asubuhi.

Miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa kuongoza zoezi hilo ni mkuu wa mkoa wa Mtwara atakayeambatana na wakuu wa wilaya za mkoa wa Mtwara pamoja na wakurugenzi wa wilaya,manispaa na miji mkoani humo.

Shughuli kubwa itakuwa ni kufanya usafi wa mazingira kwenye maeneo mbalimbali ya Mji kwa kushirikisha timu ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, viongozi mbalimbali ngazi za Wilaya, Halmashauri, kata, vijiji na mitaa ikiwa ni pamoja na wananchi wote wa Masasi.

Katika siku  hiyo shughuli zote za kiofisi, kijamii na kibiashara zitasimama kipindi chote cha zoezi hilo ili kuruhusu wananchi wote kushiriki kikamilifu kufanya usafi wa mazingira kwenye maeneo yao.

Shughuli za usafi wa mazingira zitaanza rasmi tarehe 25/7/2016 na zitaendelea mpaka siku ya kilele yaani tarehe 30/7/2016 ambapo wananchi wote watafanya usafi kwenye maeneo yao ya makazi na biashara.

Kwa upande wa Halmashauri ya Mji wa Masasi tayari maandalizi yameshaanza ikiwa ni pamoja na kufanya uhamasishaji jamii kwa njia ya matangazo ya gari, Radio, Ujumbe mfupi wa simu za mkononi, matangazo ya mabango ya vitambaa yatakayowekwa kwenye njia kuu, kutoa matangazo kwenye nyumba za ibada pamoja na kuongea na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa.

Baadhi ya Viongozi wa vyama vya siasa akiwemo  Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Masasi na waheshimiwa madiwani wote wa jimbo la Masasi watashirikishwa kikamlifu katika kufanikisha zoezi hili la usafi wa mji wa Masasi lakini pia  watu maarufu kwenye jamii na maafisa watendaji wa kata na mitaa wote watashiriki kuhamasisha jamii.

Ewe Mkazi wa mji wa Masasi jitokeze kufanya usafi pamoja na mkuu wa mkoa wa Mtwara siku ya tarehe 30/07/2016 kuanzia saa 12:00 Asubuhi hadi saa 4:00 Asubuhi.

kauli mbiu:  “Ona aibu kuishi na uchafu, ifanye Masasi iwe safi”









TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top