Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

WAZIRI MKUU MH:KASSIM MAJALIWA KASSIM KUANZA ZIARA YA SIKU TATU KESHO RUANGWA

TANGAZO


Na Bashiru Kauchumbe,Ruangwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi Mhe Kassimu Majaliwa kesho anatarajia kuanza  ziara ya siku tatu Wilayani Ruangwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mariamu Mtima alisema  ziara hiyo ya kikazi itaanza kesho jumapili ya April 10,2016.

Katika ziara hiyo Majaliwa atapokelewa na Uongozi wa Wilaya ya Ruangwa katika kijiji cha Likunja majira ya saa 9.30 alasili ambapo atapata fursa ya kuongea na  wananchi wa kijiji hicho na kwamba Pia siku hiyo hiyo ataongea na wananchi wa kijiji cha Kitandi majira ya saa 11:00 za jioni.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya alisema  Siku ya pili ya ziara yake Mh: Majaliwa ataweka jiwe la msingi jengo la Bohari ndogo ya kuhifadhia  Madawa katika Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa pamoja na uzinduzi wa chumba cha kutunzia watoto waliozaliwa wakiwa njiti.

Aidha atatembelea  katika Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa kwa lengo la  kuona wagonjwa pamoja na kuangalia mazingira ya utendaji kazi katika Hospitali hiyo,Majaliwa atakamilisha ziara yake siku ya pili kwa kutembelea Soko kuu la Wilayani humo na mwisho ataongea na watumishi wa Wilaya ya Ruangwa.

Siku ya tatu ya ziara yake waziri mkuu huyo atapata nafasi ya kuongea na wanawake wa wilaya ya Ruangwa  katika ukumbi wa chama cha walimu wilayani humo.


Katika ziara hiyo waziri mkuu Mh: Kasimu Majaliwa atafanya mikutano ya hadhara katika vijiji vya Nkowe,Luchelegwa ,Chinongwe na Nanganga na hatimaye kuondoka kuelekea Mjini Lindi.



TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top