Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

Mwanamke Ruangwa Apata Ulemavu Wa Macho Baada ya Kupigwa Na Wanaume Wawili Tofauti.

TANGAZO
Na Bashiru Kauchumbe,Ruangwa.
MKAZI wa kijiji cha Dodoma wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi Alapha Matingo (40)  amepoteza baadhi ya viungo vyake ikiwemo macho yake baada ya kufanyiwa vitendo vya kikatili ikiwemo kipigo kutoka kwa wanaume wawili tofauti.
Akisimulia mkasa huo Matingo alisema mwaka 2007 akiwa anaishi  na mume wake aliyejulikana kwa jina la Kiweru Abdallah  Mkazi wa Kilimahewa wilayani alipigwa vibaya na mume wake baada ya kuhoji tabia ya mume huyo kurudi usiku wa manane akiwa amelewa.
Alisema kutokana na kipigo hicho jicho lake moja la upande wa kushoto lilipata majeraha makubwa na hatimaye kupasuka na alikimbizwa katika hosiptali ya rufaa ya Ndanda wilayani Masasi ambako hata hivyo jicho hilo halikuweza kuona tena na kuwekewa jicho la bandia.
“Ilikuwa ni siku ambayo siwezi kuisahau katika maisha yangu…mume wangu alirudi nyumbani usiku majira ya saa 5:00 akiwa amelewa na bila kuuliza chochote alianza kunipiga mwili mzima na akafanikiwa kupasua jicho langu la kushoto nilikimbizwa hospitali lakini madaktari hawakufanikiwa kutibu na hatimaye waliniwekea jicho la bandia”alisema Matingo.
Alisema baada ya tukio hilo mume wake alikamatwa na jeshi la polisi wilayani Ruangwa na kufikishwa mahakamani ambapo alifungwa kifungo cha miaka mitatu jela.
Kwa mujibu wa Alapha Matingo alisema mwanzoni mwa mwaka 2012, aliolewa tena na mume mwingine aliyejulikana kwa jina la Ndoje Athumani ambapo Desemba mwaka huo alikumbwa na mkasa mwingine wa kupigwa vibaya kwenye jicho lake la pili lililopasuka papo hapo.
Alisema kipigo hiko kilimsababishia mauimvu makali na hatimaye jicho lake kuondolewa na kubaki mlemavu wa macho hadi sasa mazingira yaliyomsababishia kuishi katika mazingira magumu kutokana na ulemavu huo wa macho.
Alisema katika hatua isiyo kuwa ya kawaida mume wake huyo hakuchukuliwa hatua zozote za kisheria na ameendelea kufurahia maisha huku yeye akiwa anaishi kwa shida kwa kutokuona kwake huku jukumu la kumtunza mume wake huyo likibaki kuwa lake.
Kwa upande wake Ndoje Athumani ambaye hadi leo hii anaishi na mke wake huyo mlemavu wa macho alipotakiwa kutoa maelezo alikiri kutenda kosa hilo huku akijutia maamuzi hayo ambapo alisema kilichosababisha kufanya maamuzi hayo ni unywaji wake wa pombe kupita kiasi huku akitoa ahadi ya kutomuacha mke huyo  hadi mwisho wa maisha yake.


TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top