Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

KIONGOZI WA MASHTAKA NCHINI ITALIA ATAKA KOCHA MPYA WA CHELSEA AHUKUMIWE JELA

TANGAZO
Kocha Mpya wa Chelsea Antonio Conte.
Kiongozi wa mashtaka nchini Italia amependekeza kocha mpya wa Chelsea Antonio Conte kuhukumiwa kifungo cha miezi 6 kwa mchango wake katika kupanga mechi mwaka wa 2011.
Wakili wa Conte amesisitiza kuwa mteja wake hakufanya kosa lolote.
Kocha huyo mpya wa Chelsea anakabiliwa na tuhuma za ''udanganyifu katika michezo'' katika mji wa Cremona Italia.
Kesi hiyo inahusiana na madai kuwa klabu ya ligi ya daraja la pili Serie B.;Siena aliyokuwa akiifunza mnamo mwaka wa 2011 ilihusishwa na kashfa ya upangaji mechi.
Konte mwenye umri wa miaka 46 pia aliwahi kuifunza Juventus.
Aliwashangaza wengi alipoteuliwa meneja mkuu Stamford bridge baada ya kuiongoza Italia katika mashindano ya Euro.
Tayari kocha huyo ametumikia marufuku ya shirikisho la soka la Italia kuhusiana na tukio hilo la mwaka wa 2011.
Kiongozi wa mashtaka Roberto di Martino, ametaja mechi kati ya klabu yake na timu ya Albino Leffe, ambayo anadai Conte alifahamu fika jaribio la kupanga matokeo yake.
Amependekeza Conte ahukumiwe kifungo cha miezi 6 na kutozwa fain ya euro 8,000.
Wakili wa Conte , Leonardo Cammarata, anatarajiwa kumtetea mteja wake Aprili 11.
Mahakama itatoa uamuzi wake mwezi Mei.
Msemaji wa waajiri wapya wa Conte Chelsea alikataa kuzungumzia swala hilo.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top