Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

DIWANI KATA YA MICHIGA AKABIDHI VIFAA VYA UZAZI KWA KITUO CHA AFYA CHA MICHIGA

TANGAZO
 DIWANI wa kata ya Michiga Hashimu Nassir (Kulia) akikabidhi mabeseni kwa kaimu mkuu wa kituo cha Afya cha Michiga Jofrey Jally ikiwa ni miongoni mwa vifaa alivyovikabidhi hii leo.

Na Clarence Chilumba, Nanyumbu.
DIWANI wa kata ya Michiga jimbo la Nanyumbu mkoani Mtwara,Hashimu Nassir (CCM)  amenunua vifaa vya kujifungulia akinamama wajawazito vyenye thamani ya shilingi laki saba  ambapo kila mjazito ambaye yupo katika kata hiyo atahudumiwa bure  kwa kutumia vifaa hivyo pale anapoenda kujifungua.

Vifaa alivyonunua na kuvikabidhi leo katika kituo cha afya cha Michiga ni pamoja groves za kuvaa mikokoni,beseni za kuwekea maji,sindano  pamoja na nailoni ngumu ambazo mama mjamzito hutandika wakati anapojiandaa kujifungua.

Pia diwani huyo amekabidhi vifaa vya mfumo wa umeme jua (Solar) katika kituo hicho cha afya kwa lengo la kuondoa kero iliyodumu kwa muda wa miaka miwili iliyowalazimu wajawazito kujifungulia kwa kutumia mwanga wa tochi za simu nyakati za usiku.

Diwani huyo ameamua kununua vifaa hivyo kwa fedha zake za mfukoni kwa lengo la kuwaondolea kero  akinamama wajawazito pamoja na wananchi kwa ujumla wanaopata huduma katika kituo hiko ambapo awali  akinamama hao walijifungulia gizani sambamba na kutakiwa kubeba vifaa vya kujifungulia.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo,diwani huyo alisema huu ni wakati wa viongozi wa kisiasa na serikali kutekeleza ahadi walizoziahidi kwa wananchi wakati wanaomba kuchaguliwa na kwamba ataendelea kufanya hivyo katika kipindi chote cha uongozi wake.

 “Nimeguswa na tatizo la wajawazito wanapokwenda pale kwenye kituo cha afya nyakati kujifungua gizani huku wakilazimika kutumia mwanga wa simu na vibatari…mbaya zaidi ni pale wanapoelezwa   kuwa hakuna vifaa vya kujifungulia na kutakiwa wakanunue wenyewe ndio maana nimeamua kununua kwa ajili ya wajawazito wa kata yangu”.alisema Nassir.

Alisema kituo hiko ni muhimu kwa wananchi wengi wa maeneo hayo hata wale wa wilaya jirani ya Tunduru mkoani Ruvuma ambapo ameiomba serikali ya awamu ya tano kukiangalia kituo hiko kwa jicho la tatu ili kiweze kutoa huduma bora kwa wwananchi hao.

Kwa upande wake kaimu mkuu wa kituo cha afya cha Michiga Jofrey Jally alisema kituo hiko chenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa 90 hadi 100 kwa siku kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa dawa,jumba la wagonjwa,ukosefu wa miundo mbinu rafiki kwa wagonjwa pamoja na uzio kwa ajili ya usalama.

Alisema kutokana na kituo hiko kuhudumia wagonjwa wengi kutoka katika vijiji vya Michiga,Pachani,Mnazimmoja pamoja na Nandembo kumesababisha kuwepo na mlundikano wa wagonjwa na hivyo kushindwa kutoa huduma kikamilifu.

“Licha ya kituo hiki kuhudumia wagonjwa kutoka katika vijiji hivyo…pia tunapokea wagonjwa wengine kutoka katika vijiji vyenye zahanati ambao wameshindwa kuwahudumia na vijiji hivyo ni Makong’onda,Lumesule,Nakopi,Mburusa na Likokona”alisema Jally.

Kituo cha afya cha Michiga,kata ya Michiga,Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara ni miongoni mwa vituo vikubwa wilayani humo huku kikiwa kinakabiliwa na changamoto mbalimbali.


 BAADHI ya watumishi wa kituo cha afya cha Michiga pamoja na wananchi wa kata hiyo wakimsikiliza diwani wa kata hiyo (hayuko pichani) wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa kitu hiko.

 DIWANI wa kata ya Michiga Hashimu Nassir akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo.
 BAADHI ya wagonjwa wakiwa wamelala kwenye moja ya wodi iliyofungwa mfumo wa umeme jua vifaa vilivyonunuliwa na diwani wa kata hiyo ya Michiga Hashim Nassir.
 MZEE Moizi Nkakia akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa kata ya Michiga baada ya diwani kukabidhi vifaa hivyo.
 KAIMU mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nanyumbu Bwana Ajika akizungumza wakati wa tafrija ya kukabidhi vifaa katika kituo cha afya cha Michiga.
Diwani wa kata ya Michiga na kaimu mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nanyumbu Bwana Ajika wakipata maelezo kutoka kwa mganga wa kituo hiko kwenye chumba cha upasuaji katika kituo hiko cha afya.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top