Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

TAARIFA KWA WAMILIKI WOTE WA VYOMBO VYA USAFIRISHAJI PIKIPIKI MAGURUDUMU MAWILI NA MATATU.

TANGAZO

HALMASHAURI YA MJI MASASI 
 TAARIFA KWA WAMILIKI WOTE WA VYOMBO VYA USAFIRISHAJI PIKIPIKI MAGURUDUMU MAWILI NA MATATU.

Serikali kupitia bunge lake la kumi ilipitisha kanuni za Leseni za usafirishaji wa abiria kwa njia ya pikipiki za magurudumu mawili na matatu (The Transport Licensing (motorcycles an tricycles) regulation 2010.

Kanuni hizo zimezipa mamlaka za serikali za mitaa kutoa leseni za usafirishaji wa abiria kwa kutumia pikipiki za miguu miwili na mitatu kwa makubaliano maalumu na SUMATRA (Memorandum of Understanding)

Kufuatia makubaliano hayo Halmashauri ya Mji Masasi inaanza kutekeleza Sheria Chini ya Kifungu 5A cha Sheria ya SUMATRA Na. 9 ya 2001 na kanuni za Leseni za usafirishaji Pikipiki magurudumu mawili (Bodaboda) na matatu (Bajaji) kuanzia sasa.

Leseni za usafirishaji (SUMATRA) zinapatikana katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji kuanzia sasa.

MASHARTI YA KUPATA LESENI YA USAFIRISHAJI PIKIPIKI NA BAJAJI
1.    Barua ya maombi ya leseni (aoneshe kijiwe anachotoka/ anachopaki)
2.    Barua ya utambulisho kutoka serikali ya Mtaa.
3.    Nakala ya kadi ya  pikipiki/ bajaji
4.    Nakala ya Bima ya pikipiki/ bajaji
5.    Nakala ya leseni ya udereva
6.    Taarifa ya ukaguzi wa chombo cha usafirishaji kutoka polisi (vehicle inspection report)

ADA YA LESENI YA USAFIRISHAJI                                                
1.   PIKIPIKI: Fomu ya maombi ni Tshs 2,000/= na Ada ya leseni kwa mwaka ni Tshs 20,000/=
 JUMLA SHILINGI 22,000/=

2.   BAJAJI: Fomu ya maombi ni Tshs 2,000/= na Ada ya leseni kwa mwaka ni Tshs 30,000/ JUMLA SHILINGI 32,000/=

Malipo yote yanafanyika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mji Masasi.
VIJIWE VINAVYOTAMBULIKA MPAKA SASA NI VIFUATAVYO;
1.    Resti camp, Mkomaindo na barabara ya Tunduru
2.    Eneo la Stendi na barabara ya Nachingwea
3.    Eneo la Mkuti sokoni, kaumu, eneo la machinjioni
4.    Jida na mtandi
5.    TK, eneo  la Nyasa Magengeni na Barabara ya Newala.

SHERIA NA KANUNI ZA UTEKELEZAJI
Kila mmiliki wa chombo cha kusafirisha abiria kwa kutumia Bodaboda na Bajaji ni wajibu chombo chake kukilipia Leseni ya Usafirishaji. Kutakuwa na msako mkali kwa waendesha pikipiki na Bajaji ambao utashirikisha Maafisa wa SUMATRA na Jeshi la polisi ili kuwabaini wote ambao watakuwa wanakeuka sheria hii na kanuni za usafirishaji wa abiria kwa kutumia Pikipiki na Bajaji/ Guta kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Tunatoa wito kwa wamiliki wote wa vyombo vya usafirishaji (Pikipiki, Bajaji na Guta) kuvikatia haraka Leseni vyombo vyenu ili kuepukana na usumbufu pindi operesheni ya kudumu ya ukaguzi wa vyombo hivyo.

CHINI YA KIFUNGU 5A CHA SHERIA YA SUMATRA NA. 9 YA 2001
Masharti ya leseni za pikipiki kwa mujibu wa Kanuni namba 13,14 na 15 ya Kanuni za Leseni ya Usafirishaji kwa kutumia Pikipiki yatamhitaji mmiliki wa leseni kuhakikisha kwamba:
1.    Pikipiki ya abiria inakuwa katika hali ya usalama na ubora
2.    Derive wa pikipiki ana leseni inayomruhusu kuendesha pikipiki husika
3.    Pikipiki ya magurudumu mawili haibebi zaidi ya abiria mmoja
4.    Dereva wa pikipiki anavaa sare safi na nadhifu na abandike kitambulisho mahali kinapoweza kuonekana na mtu yoyote
5.    Dereva wa pikipiki azingatie vikomo vya kasi ya mwendo uliowekwa
6.    Dereva wa pikipiki ya abiria avae kofia ngumu (Helmet) yenye namba ya utambulisho wakati wote anapoendesha pikipiki
7.    Dereva wa pikipiki ahakikishe kuwa abiria wake amevaa kofia ngumu wakati wote wa safari
8.    Dereva wa pikipiki haruhusiwi kutumia simu ya mkononi wakati wote anapoendesha
9.    Dereva wa pikipiki za magurudumu mawili haruhusiwi kubeba abiria mwenye umri chini ya miaka tisa (9)
10. Dereva wa pikipiki akiwa kazini asifanye vitendo vifuatavyo
a)    Kutumia lugha ya uhasama au matusi kwa abiria
b)   Kuendesha pikipiki akiwa amekunywa pombe au kutumia madawa ya kulevya
c)    Kuendesha pikipiki kwa uzembe au namna ya hatari au kinyume na sheria ya usalama barabarani na sheria zingine.

Kwa maelezo zaidi fika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mji Masasi.

Clarence Chilumba,
Ofisa Habari Halmashauri ya Mji
MASASI.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top