TANGAZO
![]() |
Mwenyekiti wa MTPC Hassan Simba |
Na Fatuma Maumba,Mtwara
Waandishi wa habari nchini wametakiwa
kuandika habari za vijijini ambazo zimekuwa haziandikwi kwa kiwango
kinachostahili na badala yake wamekuwa wakiandika habari nyingi za mjini
kuliko za vijijini.
Hayo yalisemwa hivi karibuni, mjini
hapa na Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa Habari mkoani Mtwara (MTPC),
Hassani Simba, wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa katika
kikao cha kawaida cha kukumbushana juu ya utendaji kazi wa waandishi hao.
Aidha,Simba alieleza kwamba waandishi
wengi wamekuwa wakijikita kuandika habari za mjini pekee wakati kuna kundi
kubwa la watu ambalo linaishi vijijini likikosa huduma mbalimbali za kijamii,
hususani afya , miundombinu na maji safi na salama.
Alisema wanahabari wanauwezo mkubwa sana wa kuandika habari za
vijijini na wakaibua matatizo makubwa sana na changamoto zake katika jamii
lakini watu hao wamewasahau kabisa kuandika habari zao .
“Waandishi wa habari tumewasahau
wananchi wanaoishi vijijini tukumbuke ya kwamba kundi hili wanatutegemea sisi
tupamze sauti zao kwa kuwaandikia matatizo walikuwa nayo, kwani wao hawana
sehemu pa kusemea zaidi ya kututegemea sisi kuibua matatizo yao” Alisema Simba.
Simba alisisitiza ya kwamba waandishi
wa habari pia wakumbuke kuandika habari zenye uwiano sawa habari za mjini na
vijijini bila kuleta upendeleo wowote hule kwani watakapoandika usawa
habari hizo zitaleta furaha kwa kundi hilo ambalo limesahaulika na kujiona
kwamba nao wanathaminiwa.
Ikumbukwe ya kwamba kundi kubwa
linaloishi vijijini wengi wao ni maskini na hawana sauti kabisa kwaiyo ni
jukumu lao wao kama waandishi wa habari kuwasemea wananchi wasiokua na
sauti kwani jamii hiyo inawategemea sana wanahabari kwa asilimia mia
moja.
Simba alisema, hakuna sehemu yoyote ile ambayo inayoendelea ama
kupata mafanikio bila kuwa na vyombo vya habari kwa hiyo naomba wajitaidi sana
wanahabari kuandika habari za vijijini ili kuleta maendeleo sehemu hiyo.
“Tunapaswa kuwafikia wananchi ambao
wanaishi vijijini wanaohitaji habari za kusoma kwenye magazeti,
kusikiliza redio na kutazama Luninga juu ya taarifa zao za vijijini ili kuweza
kupata motisha ya maendeleo yao kiujumla” Alisema Simba.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD