TANGAZO
Na Clarence Chilumba,Masasi.
IMEBAINIKA kuwa baadhi ya
wafanyabiashara wa eneo la stendi kuu ya mabasi mjini Masasi wasiokuwa na vitendo vya kiustaharabu wamekuwa
na tabia ya kujisaidia haja ndogo (MKOJO) kwenye chupa za maji na hatimaye
kutupa chupa hizo kwenye vichochoro vilivyopo katika mabanda yao ya biashara.
Uchunguzi uliofanywa na “MTAZAMO MPYA” umebaini kuwa
maeneo mengi yenye vichochoro katikati ya mabanda yaliyopo stendi kuu ya mabasi
mjini Masasi yamekuwa maficho ya uchafu na vyupa vya mkojo na mengine hata
kinyesi cha binadamu hupatikana.
Aidha tabia nyingine iliyobainika ni
kuwepo kwa uchafu kwenye mifereji inayopitisha maji machafu kunakosababishwa na
baadhi ya wafanyabiashara hao kutupa takataka kama vile chupa tupu za
maji,mifuko ya plastiki,pamoja na matairi yaliyoisha kwenye mifereji hiyo.
Hayo yamebainika leo wakati wa zoezi la
usafi linaloendelea kufanywa kwenye maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya mji wa
Masasi katika maadhimisho ya wiki ya Wanawake duniani yaliyoanza siku ya
jumapili na yanatarajia kukamilika ifikapo machi nane 2015.
Wakizungumza baadhi ya
wafanyabiashara hao wamestushwa kuwepo kwa vitendo hivyo visivyo vya kiungwana
na kwamba hawajui ni nani amekuwa na tabia hiyo licha ya kuhaidi kuendelea
kuwatafuta wanaohusika na uchafuzi huo.
Katika Hatua nyingine chama cha mawakala
wa usafirishaji abiria katika magari yaendayo mikoani na wilayani kimeanzisha
utaratibu wa usafi kwenye eneo hilo la stendi kwa kudhibiti wote wanaotupa
uchafu kwenye eneo hilo na kwamba yeyote atakayebainika hatua kali
zitachukuliwa dhidi yake.
Miongoni mwa mikakati iliyopo ni
pamoja na kuhakikisha kuwa takataka zote zinawekwa kwenye eneo maalumu la
kukusanyia ili wafanyakazi wa Halmashauri ya mji wa Masasi wanaozoa taka wazoe
kwa urahisi.
WITO: JUKUMU LA USAFI
SI LA HALMASHAURI PEKEE,NI LA KILA MWANANCHI WA MJI WA MASASI.HAKIKA
TUKISHIRIKIANA KIKAMILIFU MJI WA MASASI UTAKUWA MSAFI WAKATI WOTE KWA FAIDA
YETU WOTE.
“AIDHA MKURUGENZI WA
HALMASHAURI YA MJI WA MASASI ANAWAKUMBUSHA KUWA KILA IFIKAPO JUMAMOSI YA MWISHO
WA MWEZI ITAKUWA NI SIKU YA USAFI”
Chupa zenye mkojo zilizokutwa kwenye mabanda yaliyopo kwenye eneo la stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na wilayani katika mji wa Masasi zilizotupwa na wafanyabiashara wa eneo hilo.
Akinamama wakiwa kwenye zoezi la usafi linaloendelea mjini masasi wakiondoa chupa pamoja na mifuko ya plastiki iliyotupwa kwenye mifereji inayopitisha maji machafu katika eneo la stendi kuu ya mabasi mjini Masasi katika kuadhimisha maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani.
Mzee ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa kwenye zoezi la usafi wa mazingira hii leo katika eneo la stendi kuu ya mabasi mjini Masasi.
Akinamama waliojitokeza kwenye zoezi la usafi wakiwa wameshikwa na mshtuko baada ya kukuta matairi yaliyoisha yakiwa yametupwa ndani ya mifereji inayopitisha maji machafu katika eneo la stendi kuu ya mabasi mjini masasi wakati wa zoezi la usafi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD