TANGAZO
Na Clarence Chilumba,Masasi.
Wazazi wapatao 23 wakazi wa kata za
Mpindimbi na Lukuledi wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wamepandishwa
kizimbani kujibu shitaka linalowakabili la kushindwa kupeleka watoto wao shuleni
waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo wa 2014/2015.
Watuhumiwa hao wamefikishwa katika mahakama ya mwanzo ya
Lisekese hii leo jumatatu kujibu shitaka hilo walilotenda kwa
makusudi huku wakijua ni kosa linalokwenda kinyume na sheria ya mtoto ya mwaka
2009.
Mbele ya hakimu wa mahakama ya mwanzo ya
Lisekese watuhumiwa 20 walikiri kosa hilo huku watatu wakikana shitaka hilo
ambao kwa mujibu wa sheria kesi yao itaendelea kusikilizwa.
Katika shitaka hilo
la kushindwa kutimiza majukumu yao kwa watoto wao ikiwemo elimu watuhumiwa 19
wametupwa rumande huku wanne wakipewa dhamana.
Hakimu wa mahakama ya
mwanzo ya Lisekese alihairisha kesi hiyo hadi machi 25 2015 itakapotolewa
hukumu yake huku watuhumiwa hao 19 wakibaki rumande.
Kufikishwa mahakamani
kwa wazazi hao kumekuja ikiwa ni utekelezaji wa agizo alilolitoa mkuu wa mkoa
wa Mtwara Halima Dendego wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa maabara
aliyoifanya wilayani Masasi ambapo aliwaagiza watendaji wa kata,vijiji na mitaa
kuhakikisha kuwa watoto wote wanaripoti shuleni.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD