TANGAZO
Na Clarence Chilumba,Masasi.
Jeshi la polisi mkoani Mtwara,
linawashikilia watu wawili Shaha Saidi (45) na Shedrack Alaya (47) fundi seremala mkazi wa Mkuti, kwa kosa la kusafirisha pakiti
166 za milipuko aina ya Super power 90 emulsion explosive ndani ya basi kinyume na sheria.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Augustino Ollomi, alisema tukio hilo
lilitokea Februari 19 mwaka huu majira ya saa 4:00 asubuhi maeneo ya Miesi, Kata ya Maendeleo,
Tarafa ya Lisekese wilayani Masasi.
Kamanda Ollomi, alisema mtuhumiwa Shaha Saidi alibainika baada
ya askari waliokuwa doria kufanya upekuzi ndani ya basi hilo na kubaini kuwa
mtuhumiwa alikuwa anasafirisha milipuko hiyo kwenye boksi kisha kuiweka kwenye
mfuko wa salfeti.
Kwa mujibu wa Ollomi alisema kwamba
upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea na kwamba jeshi la polisi mkoani Mtwara linawashukuru
wananchi wote ambao wamekuwa wakishirikiana na jeshi hilo kwa kutoa taarifa za
kufichua wahalifu na linawaomba wazidi kuongeza ushirikiano huo ili waweze
kukomesha vitendo vya uhalifu.
Wakati huo huo Jeshi hilo linatoa
tahadhari kwa wamiliki na waendesha pikipiki kuwa makini kutokana na wizi wa
pikipiki unaotokea maeneo ya uwanja wa Nangwanda Sijaona kunapofanyika
michezo ya mpira wa miguu.
Kamanda Ollomi alisema taarifa
zimeripotiwa polisi zinaonyesha kwamba katika michezo yote mitatu ya mpira wa
miguu ya hivi karibuni iliyofanyika uwanjani hapo kumetokea na wizi wa
pikipiki.
“Jeshi la polisi mkoa wa Mtwara
linawatahadharisha wamiliki na madereva pikipiki kuchukua tahadhari au kuepuka
kuegesha pikipiki zao nje ya uwanja huo huku wao wakiingia ndani kuangalia
mpira kwani watu wote walioibiwa pikipiki zao waliziacha nje ya uwanja huo nao
kuingia ndani kuangalia mpira na walipotoka nje hawakukuta pikipiki.
Jeshi la polisi linaendelea na upekuzi kwa matukio yote
hayo ya wizi wa pikipiki yaliyoripotiwa na pia imewaomba wananchi wote ikiwa
wana taarifa za mtu au kikundi cha watu wanaojihusisha na uhalifu huo waripoti
polisi ili hatua za haraka za ziweze kuchukuliwa na watuhumiwa waweze
kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD