Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

SHULE 14 HALMASHAURI YA MJI MASASI ZANUFAIKA NA MGAO WA MADAWATI YA KISASA

TANGAZO
 Na Clarence Chilumba,Masasi.

Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara  kupitia idara ya elimu msingi imepokea madawati 617 ya plastiki kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  yaliyonunuliwa  kutokana na chenji ya ununuzi wa Rada iliyorudishiwa serikali ya Tanzania kutoka serikali ya uingereza.

Hayo yalisemwa leo  na Ofisa elimu msingi Halmashauri ya mji masasi Mzenga Twalibu wakati anawasilisha taarifa yake kwenye kikao cha kamati ya fedha na utawala ya Halmashauri hiyo.

Alisema  madawati 370 ni maalumu kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la kwanza hadi darasa la nne kwa madawati ya rangi ya bluu huku  madawati 247 wakipewa  wanafunzi wa darasa la tano na darasa la  saba ili waweze kufanya vizuri mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi.

Kwa mujibu wa Mzenga alisema  tayari idara yake imeshagawa madawati hayo kwa shule 14 kati ya 20 zenye upungufu mkubwa sana wa madawati. 

 Baadhi ya MADAWATI hayo ya plastiki ngumu 
 Mafundi wa kampuni ya JAMBO PLASTIKI wakifunga madawati hayo



Ofisa Elimu Msingi Halmashauri ya Mji wa Masasi Mzenga Twalibu Mzenga wakati anaongea na waandishi wa Habari (Hawako Pichani) wakati anatoa taarifa ya mapokezi ya Madawati hayo.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top