TANGAZO
Na Haika Kimaro,Mtwara.
Mkuu
wa mkoa wa Mtwara Halima Dendegu ameuagiza uongozi wa Hospitali ya mkoa ya Ligula
kuhakikisha inafuata miongozo na kanuni za usafi katika hospitali hiyo ambayo
kwa sasa imekithiri kwa uchafu.
Aidha
amesikitishwa kuona hospitali hiyo yenye hadhi ya rufaa kukithiri kwa uchafu
kuanzia mazingira ya nje, vyoo hadi kwenye wodi za wagonjwa huku uongozi wa
hospitali hiyo ukiwa haujachukua hatua zozote za kuinusuru hali hiyo.
Pia mkuu huyo wa mkoa ameshangazwa na na hali ya wauguzi (manesi) wa hospitali hiyo kutokuzingatia maadili ya taaluma yao mara
baada ya kukuta wakiwa wamevaa ndala kinyume
na taratibu za mavazi ya utumishi wa umma hali inayosababisha wagonjwa kukata tamaa.
Kutokana
na hali hiyo Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mtwara Ligula iko hatarini kukumbwa
na magonjwa ya milipuko kufuatia kuwa katika hali ya uchafu katika maeneo mengi
ya hospitali hiyo kuanzia nje hadi wodini.
Dendegu
aliyasema hayo juzi wakati wa kikao cha mazingira baada ya kufanya ukaguzi wa
kushtukiza kwenye hospitali hiyo ambapo alikuta wagonjwa wakiwa katika hali mbaya
huku baadhi ya wauguzi wakifanya shughuli zao ikiwa ni pamoja na kuongea na simu
(Kuchati) badala ya kufanya kazi zilizowapeleka hospitalini hapo.
Alisema
hali iliyopo katika hosiptali hiyo si ya kuridhisha na kwamba alidai kukuta
nyasi zikiwa zimeota hadi kwenye madirisha, vyoo vya nje vikiwa vichafu huku
baadhi ya wagonjwa wodini wakiwa wanalalia mipira kwa madai kuwa shuka ni chafu
huku vifaa vya kufulia navyo vikiwa vichafu sambamba vyoo vinavyotumiwa na
wagonjwa hao.
“Nakuagiza
mganga mkuu zile sheria za utumishi wa umma zifuatwe nendeni miongozo ibandikwe
nesi anatakiwa kuwa vipi mtu yuko busy na simu wagonjwa wanakosa huduma,
hivi mtu mwanae akifa kwa uzembe utasema nini?”.alihoji Dendegu.
Alisema watu wanafanya kazi kwa mazoea na
utafikiri wako mtaani na kwamba matokeo
ya uzembe huo ni lawama kwa serikali
kuwa imeshindwa kutoa huduma bora kwa wananchi wake hakika hili halipaswi
kuachwa hivi hivi.
Aidha
alikiri ni kweli kuwa watumishi katika hospitali hiyo ni wachache ambapo
alisema hao wachache waliopo ni lazima wafanye kazi kwa bidii wakati serikali
inafanya taratibu za kupeleka watumishi.
Aidha
alisema kuwa fahari yake ni kuona kila mtu anafanya kazi yake na kuwataka wakuu
wote wa wilaya pamoja na madiwani kuwajibika katika suala nzima la usafi wa
mazingira kwa wao kuanza kuonesha mfano.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD