TANGAZO
Na Clarence Chilumba, Masasi.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego jana aliwaongoza mamia ya waombolezaji waliojitokeza katika mazishi ya aliyekuwa dereva wa mkuu wa mkoa wa Mtwara Gaudence Mkapa (53).
Marehemu Mkapa alifariki februari 21 mwaka huu majira ya saa 5:00 asubuhi katika hospitali ya rufaa ya Muhimbili mkoani Dar es salaam alikolazwa kutokana na matatizo ya ugonjwa wa ini na kuzikwa jana katika kijiji cha Lupaso Halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani humo.
Ibada ya kumuombea marehemu ilifanyika kwenye kanisa katoliki parokia ya Lupaso jimbo la Tunduru Masasi na kuongozwa na padre Phiniasi Amlima akisaidiwa na mapadre wengine wapatao sita Masasi na kuhudhuriwa na viongozi wa chama na serikali wilayani humo.
Akitoa salamu za serikali mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego alisema ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mtwara imempoteza mmoja wa madereva waandamizi mkoani humo waliofanya kazi kwa moyo wa kujituma katika shughuli mbalimbali alizopewa na wakuu wa mikoa sita aliowahi kufanya nao kazi.
Alisema marehemu Mkapa ni miongoni mwa madereva waliofanya kazi bila kusukumwa na aliyekuwa mwadilifu,mwaminifu na aliyefuata sala na kwamba atakumbukwa kwa mengi mazuri aliyoyanya wakati wa uhai wake ambapo ili kumuenzi ni lazima watendaji pamoja na madereva wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mtwara watekeleze majukumu yao kwa moyo wa dhati.
Kwa muijbu wa mkuu huyo wa mkoa alisema ni vigumu kwa serikali na mkoa kwa ujumla kwa sasa kuweza kuziba pengo lake ambapo amewataka madereva mkoani Mtwara kuiga utendaji kazi wa dereva mwenzao.
Marehemu wakati wa uhai wake amewahi kufanya kazi na wakuu wa mikoa wengi wakiwemo kanali Nsa Kaisi,Henry Shekifu, Isdori Shirima, kanali Joseph Simbakalia pamoja na Halima Dendego mkuu wa mkoa wa sasa.
Marehemu Mkapa alizaliwa Julai 1 1962 katika kijiji cha Lupaso wilaya ya Masasi mkoani Mtwara na alijiunga na elimu ya msingi mwaka 1969 na kuhitimu 1975 katika shule ya msingi Lupaso na baadaye alipata mafunzo ya udereva.
Baadhi ya Madereva wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa dereva mwenzao Gaudence Amandus Mkapa.
Mbunge wa jimbo la Nanyumbu Dastani Mkapa akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Gaudence Mkapa.
Mke wa marehemu akimuaga mumewe
Mama wa marehemu nae akitoa heshima za mwisho kwa mwanae Gaudence Amandus Mkapa
Hawa ni watani ambao walikuwa na mambo yao mara baada ya kurudi mazishini
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD