TANGAZO
Kaimu Katibu Tawala
Mkoa wa Mtwara Johansen Bukwali akiongea na Maafisa Mawasiliano Serikalini
ambapo alisisitiza umuhimu wa Maafisa Mawasiliano kutoa taarifa za Serikali kwa
Umma na kwa kufuata kanuni na sheria zilizowekwa.
Na Clarence Chilumba,Mtwara.
Mkuu wa
mkoa wa Mtwara Halima Dendego amekishukuru chama cha maofisa mawasiliano
serikalini kwa kutoa msaada wa vifaa kwa Hospitali ya Mkoa ya Ligula na kwamba
kwa kufanya hivyo watakuwa wameacha alama kubwa na muhimu kwa wananchi wa Mkoa
wa Mtwara.
Shukrani
hizo zimetolewa na kaimu katibu tawala wa mkoa wa Mtwara Johansen Bukwari
wakati wa kufunga kikao kazi cha maofisa mawasiliano serikalini kilichofanyika
kwa muda wa siku tano kwenye ukumbi wa NAF Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Ofisa Mawasiliano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. Atley Kuni
akitoa neno la Shukrani kwa niaba ya maofisa mawasiliano serikalini kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bw.Johansen
Bukwari kwenye ukumbi wa NAF mjini Mtwara.
Mwenyekiti wa Muda wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Innocent Mungy akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa kazi wa chama hicho
kwa Maafisa Mawasiliano wakati wa ufungaji wa kikao kazi cha Maafisa hao Mkoani Mtwara.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga akiwaeleza Maafisa Mawasiliano Serikalini umuhimu wa kuwa na ushirikiano na vyombo vya Habari kwa dhumuni la kuieleza jamii nini serikali inakifanya, pia aliwataka kuendelea kuongeza juhudi katika utendaji kazi kupitia mafunzo waliyoyapata katika kikao kazi hiko.
Baadhi ya Maafisa Mawasiliano wa Serikali
wakiwa katika picha ya Pamoja na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Johansen Bukwari (aliyevaa Kaunda suti) kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Idara
ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD