TANGAZO
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara anawatangazia wananchi wote utaratibu mpya wa usafi wa mazingira kwa mujibu wa sheria za afya ya jamii na usafi wa mazingira kama ifuatavyo:
- Kila kaya au mfanyabiashara anatakiwa kuwa na chombo cha kutunzia takataka na kukitumia kwa usahihi,ni marufuku kuchimba mashimo ya takataka.
- Kila kaya au mfanyabiashara anatakiwa kufanya usafi hadi kwenye kingo za barabara kwa wale waliopakana na barabara.
- Kila mwenye kaya au mfanyabiashara anatakiwa kusafisha mfereji wa maji ya mvua ulio mbele ya nyumba yake na kuhakikisha kuwa ni safi wakati wote.
- Ni marufuku kufanya biashara katika maeneo yaliyopo kandokando ya barabara,chini ya miti na maeneo ambayo si ya biashara.
- Ni marufuku kwa mtu yeyote kujisaidia haja ndogo au kubwa au kutupa uchafu wa aina yoyote katika maeneo ya wazi atakayekamatwa atatozwa faini ya Tsh: 50,000/= na mkamataji atalipwa asilimia 10% ya faini hiyo.
- Ni marufuku kutiririsha ovyo maji machafu kutoka chooni,bafuni,jikoni au bomba la maji machafu kuelekea kwenye barabara,uchochoroni,kwenye mfereji wa maji ya mvua ,eneo la wazi au mtoni.
- Ni marufuku kuosha magari,pikipiki au chombo chochote cha moto kwenye eneo la chanzo cha maji,eneo la wazi,kandokando ya barabara au eneo la lisiloruhusiwa.
- Kutakuwa na utaratibu wa kuzoa takatakakwa kutumia vikundi vilivyoidhinishwa na mkurugenzi wa mji ambavyo vitakuwa vikitembea kaya kwa kaya na kuzoa takataka zilizowekwa kwenye chombo maalumu. Kila mwenye kaya au mpangaji au mfanyabiashara anatakiwa kulipia gharama za uzoaji wa takataka papo kwa papo kama ifuatavyo:
- Nyumba ya kuishi Tsh:100/= kwa meta moja ya ujazo
- Majengo ya biashara na huduma Tsh: 200/=
- Biashara za rejareja Tsh: 300/= kwa meta moja ya ujazo
- Biashara za jumla Tsh: 400/= kwa meta moja ya ujazo
- Ni kosa kukataa kutoa takataka au malipo ya takataka kwa mzoaji,atakayebainika na kosa hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MJI WA MASASI.
HENRY KAGOGORO
MKURUGENZI HALMASHAURI YA MJI MASASI
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD