TANGAZO
KAYA 2944 KUNUFAIKA NA TASAF III
HALMASHAURI YA MJI MASASI.
Na Clarence Chilumba,Masasi
Mpango
wa kunusuru Kaya maskini sana kupitia awamu ya tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii- TASAF lll Halmashauri ya mji
masasi mkoani mtwara unatarajia kunufaisha Kaya zipatazo 2944 kati ya kaya 3035 zilizotarajiwa kunufaika na mpango huo.
Akizungumza
na habari leo mjini hapa Mratibu wa Tasaf
Halmashauri ya mji masasi Joram Msyangi alisema utekelezaji wa mpango
huo ambao ni kwa mara ya kwanza unatekelezwa hapa nchini ulianza kwa kuzitambua
kaya maskini sana kupitia mikutano ya hadhara ilioyofanyika katika kata na
vijiji vilivyoteuliwa.
Msyangi
alisema mara baada ya zoezi la utambuzi zilipatikana Kaya 2944 na
kila kaya itapatiwa ruzuku isiyo na masharti ya Dola tano kwa mwezi (kama
sh.8,500/),na kwamba kwa kuanzia kaya hizo zitapatiwa ruzuku ya miezi miwili.
Mratibu
huyo amezitaja changamoto mbalimbali walizokumbana nazo wakati wa zoezi la uandikishaji
wa kaya maskini sana kama vile mahudhurio duni kwenye mikutano ya hadhara
vijijini iliyochangiwa na ukosefu wa
taarifa pamoja na uwepo wa taarifa za upotoshaji kuhusu zoezi hilo
zilizozorotesha mikutano hiyo.
Changamoto
zingine zilizotajwa na Mratibu huyo wa Tasaf Halmashauri ya mji masasi ni
uelewa duni wa neno maskini hali iliyowafanya wengine wasusie kuingizwa kwenye
mpango huo kwa dhana kuwa kuitwa maskini
ni kitendo cha udhalilishaji.
Aidha
ametoa ushauri kwa Serikali kuhusu kaya zilizolengwa lakini hazikuingizwa
kwenye mpango huu.”Naishauri Serikali iangalie upya tena namna ya kuweza kuziingiza kwenye mpango ili walengwa wengi waweze kunufaika
kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini sana.”
Halmashauri
ya mji masasi ina kata 11 ambapo kati ya hizo
kata kumi ndizo zilizonufaika na mpango huo na zilianza utekelezaji wake
kwa kutambua kaya maskini mizunguko minne kisha vilimalizia kwa zoezi la
uandikishaji wa kaya maskini kwa mizunguko minne tofauti.
MWISHO
Wahusika wa mpango huo kwa ngazi ya kijiji wakiwahudumia wananchi
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD