TANGAZO
MKOMAINDO
WAZALISHA WATOTO ISHIRINI KRISMASI
Watoto wapatao ishirini
wamezaliwa wakati wa mkesha wa krismasi katika hospitali ya mkomaindo mjini
Masasi mkesha ambao wakristo kote duniani huadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa
kwa mwokozi wao yesu kristo huko katika
mji wa Bethlehemu miaka 2000 iliyopita.
Akitoa takwimu hizo
juzi muuguzi wa zamu katika hospitali hiyo ya Mkomaindo Happynes Frank alisema
kati ya watoto hao wanaume ni 12 ambapo wanawake ni wanane huku wote wakizaliwa
kwa njia ya kawaida.
Alisema hali za watoto
hao pamoja na mama zao zinaendelea vizuri na kwamba wengine tayari
wamesharuhusiwa kurudi makwao kuendelea na sherehe za krismasi na mwaka mpya.
Kwa mujibu wa muuguzi
huyo wa zamu alisema kuwa watoto hao wamezaliwa wakiwa na uzito wa zaidi ya
kilogramu mbili ambapo amekiri kuwa changamoto kubwa iliyopo ni kuwa baadhi ya
wazazi hao hukosa baadhi ya virutubisho muhimu kwenye miili yao.
Alisema kila mara
wamekuwa wakitoa elimu kwa lengo la kuwakumbusha akinamama hao umuhimu wa
kupata kinga zote pale wanapokuwa wajawazito pamoja na umuhimu wa kufanya
mazoezi na kwamba kwa kufanya hivyo kutasaidia kujifungua kwa usalama.
Mwisho.
MKOMAINDO WAZALISHA WATOTO ISHIRINI KRISMASI
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD