TANGAZO
CCM YAHAIDI KUSIMAMIA MIRADI
CHAMA
cha mapinduzi (CCM) wilayani Masasi mkoani Mtwara kimeahidi kusimamia ilani ya
chama hicho katika kuhakikisha inasimamia miradi
mbalimbali iliyotekelezwa pamoja na ile inayoendelea kutekelezwa na serikali
kuu.
Miradi
hiyo ni ile iliyotekelezwa katika
kipindi cha Julai 2013 hadi June 2014 katika sekta ya kilimo,afya,elimu,maji
pamoja na barabara na kwamba utekelezaji wake ni kwa kiwango cha asiliia 100.
Miongoni
mwa miradi hiyo ni pamoja na mradi wa
ujenzi wa daraja la Nangoo ambao umeshakamilika tangu februari 2013 na hadi
kukamilika kwake umetumia fedha za kitanzania shilingi Bilioni
4.9.
Hayo
yalisemwa mwishoni mwa wiki na mkuu wa wilaya ya Masasi Farida Mgomi wakati anawasilisha taarifa ya
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010 kwa miradi inayosimamiwa na
serikali ambapo amewata wana CCM wilayani humo kuondoa tofauti zao katika
usimamiaji wa miradi hiyo.
Kwa
mujibu wa mkuu huyo wa wilaya alisema mradi mwingine uliokamilika ni mradi wa maji
wa Mbwinji ulio chini ya Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Masasi- Nachingwea (MANAWASA) uliojengwa na kampuni ya ukandarasi ya M/S
Sinohydro Corporation Ltd ya China kwa gharama ya Bilioni 31 hadi kukamilika.
Akizungumzia kuhusu mradi wa umeme vijijini
(REA) alisema kulikuwa na miradi saba ya usambazaji wa umeme vijijini kwa awamu
ya kwanza ambapo hadi sasa vijiji saba vya
Nanganga,Nangoo,Mkalapa,Mandiwa,Mbuyuni,Matankini Pamoja na Maili sita
vimeshapatiwa umeme.
Alisema
ipo baadhi ya miradi ambayo utekelezaji
wake haujaanza rasmi kama vile mradi wa ujenzi wa barabara ya Nachingwea-Masasi-Newala-Tandahimba
ambao hadi sasa mkandarasi mshauri
ameshasaini mkataba na TANROADS
makao makuu kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina.
Alisema
mradi mwingine ambao utekelezaji wake haujaanza ni mradi wa ujenzi wa nyumba kutoka kwa shirika
la nyumba la Taifa NHC ambao tayari Halmashauri ya mji wa Masasi imeshakabidhi
eneo la Napupa mjini Masasi kwa watu wa
NHC baada ya kukidhi vigezo ikiwa ni pamoja na kulipa fidia kwa wamiliki wa
eneo hilo.
Wilaya
ya masasi mkoani mtwara ina jumla ya halmashauri mbili zenye majimbo mawili ya
uchaguzi ikiwa na tarafa sita,kata 34, vijiji 176 na vitongoji 903 ambapo kwa
sasa pato la kawaida kwa mkazi wa wilaya hiyo ni Tsh.763,0000/= kwa mwaka na
kwamba mkakati wa wilaya ni kufikia
kiasi cha Tsh. Milioni 1 kwa mwaka.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD