TANGAZO
Marehemu Daudi Mwangosi wakati wa uhai wake.
Na Mwandishi Wetu,Lindi.
Waandishi
wa habari mkoani Lindi wameungana na wenzao nchini kuadhimisha kumbukumbu ya
kuondokewa na mwanahabari mwenzao,Daud Mwangosi septemba 2,
mwaka 2012.
Katika
maadhimisho hayo ya kifo cha Mwangosi ambaye aliuawa na mlipuko wa
bomu la kutawanya watu akiwa kazini kijijini Nyalolo,mkoani Iringa ambapo wanahabari wa mkoani Lindi walikutana na wadau
mbalimbali wa habari.
Kumbukumbu
hiyo ya Mwangosi ilitanguliwa na dua ya kumwombea iliyoendeshwa na Mchungaji wa
kanisa la anglikana mjini Lindi.
Wanachama
na wadau hao walifanya mkutano katika ukumbi wa TCCIA mjini
hapa ambako walikumbushana jinsi ya kuchukua tahadhari
katika kipindi hiki cha uchaguzi ambapo kuna viashiria
vya kushambuliwa,kuteswa na kuuawa kwa wanahabari.
Mapema
akifungua mkutano huo,Katibu mtendaji wa Baraza la Habari nchini (MCT),Kajubi
Mukajanga alisema kuwa siku hiyo ni muhimu sana kwa wana habari nchini kwani inaikumbusha serikali na wadau
mbali mbali kutowazuia waandishi kutekeleza majukumu yao.
Alisema kwa kipindi cha miaka ya nyuma waandishi nchini
walikuwa wakifanya kazi bila ya hofu yoyote na kuwa tukio lililosababisha kifo
cha Mwangosi lilikuwa ni la kusikitisha kwa kuwa jambo hilo lilikuwa bado
halijawahi kutokea.
Alisema
katika kipindi hiki cha uchaguzi
ni kigumu kwa waandishi wa habari kutokana na hamasa ya uchaguzi wa mwaka huu
ambapo kwa mara ya kwanza kumekuwa na ushindani mkubwa hasa kwa wagombea wa
CCM na UKAWA hivyo kuwataka kuzingatia uweledi.
Alisema
katika kipindi hiki yapo mambo ambayo waandishi wanatakiwa kujizuia ikiwemo
kushabikia chama,kuvaa sare za vyama,kuandika habari za upande mmoja badala ya
kufanya jitihada ya kupata upande mwingine unasemaje.
Aliwaomba
waandishi wa habari katika kipindi hiki kuchukua tahadhari wakati wakitelekeza majukumu yao kwa
kuacha kufanya kazi peke yako na kujitahidi kutoa taarifa kwa mhariri au klabu
ya waandishi wa habari kuwa atakuwa wapi ili pindi itakapotokea tatizo
ifahamike.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya wanahabari mkoa wa
Lindi,akizungumza kwenye maadhimisho hayo,Christopher Lilai,alisema ili
kujinasua kutoka kwenye mazingira hatarishi wanapofanya kazi aliwataka
kuzingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.
Lilai
aliwaonya waandishi wa habari kutojihusisha na masuala ya kisiasa na kusema
kuwa kwa kufanya hivyo wengi wamekuwa wakijiweka katika mazingira hatarishi.
“Nawasihi
wanahabari wenzangu tuache kujihusisha na masuala ya kisiasa…kuwa mshabiki wa
chama fulani badala yake tuzingatie maadili yetu”alisema Lilai.
Naye Kamanda
wa polisi Mkoa wa Lindi,Renata Mzinga alisema jeshi la polisi
litatoa ushirikiano mkubwa kwa waandishi wa habari kwa kufanya kazi kwa ukaribu
na kuahidi kuwalinda wakati wote wanapotekeleza majukumu yao.
“Niwahakikishieni
ndugu zangu waandishi tupo pamoja na kuwa wiki hii nitafanya ziara
wilaya zote ili kuwaambia wenzangu wawape ushirikiano”alisema Kamanda Mzinga.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD