Loading...

MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA MTWARA ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MASASI

TANGAZO
Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mtwara Kassim Bingwe.

MWENYEKITI wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Kassim Bingwe hii leo ametangaza rasmi nia yake ya kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Masasi endapo atapewa ridhaa kutoka kwa UKAWA.
Akitangaza nia hiyo alisema lengo lake la kugombea nafasi hiyo ni kuleta maendeleo jimbo la Masasi ambalo alidai kuwa limekuwa nyuma kwa muda mrefu sasa.
Alisema haoni ni kwa nini kwa sasa wananchi wa jimbo la Masasi wasimpe ushindi ili aweze kuwahudumia ipasavyo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Aidha Bingwe alitangaza pia nia yake ya kugombea nafasi ya udiwani kata ya Mtandi Halmashauri ya mji wa Masasi.

MWENYEKITI wa CHADEMA mkoa wa Mtwara Kassim Bingwe wakati anatangaza nia ya kugombea nafasi ya Ubunge jimbo la Masasi na udiwani kata ya Mtandi hii leo kwenye viwanja vya mti Mwiba mjini Masasi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top