TANGAZO
Mkuu wa mkoa wa Mtwara HALIMA DENDEGO,leo amezindua wiki ya wanawake duniani kwa kufanya usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Ligula na kisha kuzindua zoezi la uchangiaji damu salama.
Aidha amewataka wananchi mkoani humo kujitokeza kwa wingi kwenda kuchangia damu kwenye viwanja vya mashujaa mkoani Mtwara ili kuokoa maisha ya ndugu zao,jamaa pamoja na marafiki hasa akinamama wajawazito na watoto.
Zoezi
hilo la uchngiaji damu litafanyika kwa muda wa wiki moja ambapo kilele cha
maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani kitafanyika siku ya tarehe nane mwezi
huu mkoani Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Omari Dendego akizindua wiki ya wanawake duniani kwa kuchangia damu kwenye viwanja vya mashujaa mjini Mtwara.
Wanafunzi kutoka kwenye shule mbalimbali za sekondari mkoani Mtwara nao walikuwa ni miongoni mwa watu waliochangia damu salama wakati wa uzinduzi wa wiki ya wanawake duniani.
Damu salama zikiwa kwenye mifuko yake ya kuhifadhia baada ya wachangiaji kutoa damu
Mkuu wa mkoa wa Mtwara akitoa damu kwa ajili ya kupima,kabla ya zoezi la uchangiaji damu.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akitoa maelezo kwa Daktari kabla ya kutoa damu
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD