TANGAZO
Na Clarence Chilumba,Mtwara.
Mpango wa Taifa wa
kuimarisha afya ya uzazi ili kupunguza Takwimu za vifo vya wajawazito na vifo
vya watoto wachanga kwa mwaka 2014 katika Halmashauri ya wilaya ya Mtwara zinaonesha kuwa vifo vya wanawake
vitokanavyo na uzazi ni 153 kwa kila vizazi hai 100,000.
Aidha takwimu hizo zinaonesha kuwa vifo vya watoto wachanga
vimepungua kutoka vifo 11 hadi kufikia vifo 9 kwa kila vizazi
hai 1,000.
Pia sababu kubwa zinazochangia vifo hivyo
zimetajwa ikiwa ni pamoja na kutoka damu
wakati na baada ya kujifungua kwa asilimia 77, kifafa cha mimba asilimia 26
,uambukizo asilimia 26 pamoja na ukosefu wa damu kwa asilimia 26.
Hayo yalisemwa jana na mkuu
wa wilaya ya Mtwara Wilman Ndile wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakunga
huhusu stadi za kutoa huduma za dharura kwa wanawake wajawazito na watoto
yanayoendeshwa na chama cha wakunga nchini (TAMA) kwa kushirikiana na chama cha
wakunga Canada.
Alisema mikakati ambayo Halmashauri hiyo imeweka ni
pamoja na kuhakikisha wajawazito wote katika jamii wanaandikishwa kwa kutumia
wahudumu wa afya ya uzazi.
Alisema suala la udhibiti
wa vifo kwa akinamama na watoto wachanga
ni tete nchini na ni zaidi kupita hata yale masuala ya kijamii na kwamba likifanyiwa
mzaha litasababisha vifo kuongezeka.
Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo kutoka Chama cha Wakunga
Tanzania (TAMA) Martha Rimoi alisema ujauzito sio ugonjwa lakini unaweza kuleta
ugonjwa wakati wa dharura hivyo wao wameamua kuwapa wakunga elimu ili kuokoa
maisha ya mama na mtoto.
Alisema mradi
huo umeajiri wakunga wawili waliostaafu kwa kila wilaya ili kusaidia akinamama
na kwamba watakuwa wakilipwa na mradi.
Naye mwakilishi toka chama cha wakunga nchini Canada,Esther
William alisema vifo vitokanavyo na uzazi ni moja ya changamoto kubwa ambayo
pia huchangia maendeleo kupungua.
Alisema kuwa mwaka 2011
nchi ya Canada iliamua kushirikiana na
Tanzania kuhakikisha inatokomeza vifo vitokanavyo na uzazi na kwamba mradi huo
umelenga kutoa mafunzo ya nadharia na vitendo kwa wakunga walio
kwenye vituo vya kutolea huduma katika wilaya sita.
Mafunzo hayo kwa wakunga
kuhusu stadi za kutoa huduma za dharura kwa wanawake na watoto yamelengwa kutolewa katika Halmashauri sita
ambazo ni Musoma, Morogoro,Mtwara, Mbeya, Korogwe na Ushetu.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD