TANGAZO
MAJAMBAZI YAUA MLINZI,YAPORA MILIONI 44 .
Na
Clarence Chilumba, Masasi.
Watu
wasiofahamika wamevamia na kumuuua mlinzi wa jadi katika ofisi ya chama cha
msingi cha chikundi Amcoss kilichopo katika kijiji cha Mtunungu kata ya Mwena
tarafa ya chikundi Halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara na kufanikiwa
kuiba pesa shilingi milioni 44.
Aidha
majambazi hayo yalitekeleza unyama huo kwa kuwafunga kamba mikononi na miguuni huku
wakiwaweka nguo kwenye vinywa vyao na kuwaziba kwa kutumia plasta mdomoni na puani
askari wawili wa jadi waliokuwa wanalinda ofisi hiyo ya chama cha msingi huku
mmoja wa walinzi hao akifanikiwa kujiokoa na hatimaye kukimbia.
Mlinzi
aliyeuawa kwenye tukio hilo la kinyama ni Valentino Gilbert (70) mkazi wa
chikundi na kwamba mlinzi wa pili ambaye alifanikiwa kujiokoa kwa kutumia mbinu
za kiaskari kwa maelezo yake huyo alitambuliwa kwa jina la Bakari Ibrahimu (40).
Tukio
hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 9:30 Alfajiri huko katika
kijiji cha Mtunungu kwenye ofisi ya chama cha msingi cha chikundi ambapo kundi
la watu wasiofahamika wakiwa na silaha walivamia ofisi hiyo na kuvunja na
hatimaye kufanikiwa kuondoka na fedha shilingi milioni 44 mali ya chikundi
Amcoss.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Mtwara Augustino Ollomi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema
usiku wa kuamkia leo majira ya saa 9:30 alfajiri kundi hilo la watu
wanaosadikiwa kuwa wanne walivamia ofisi hiyo na kumuua mlinzi mmoja huku
mlinzi wa pili akifanikiwa kujiokoa.
Alisema
majambazi hayo yaliyokuwa na silaha yaliwavamia walinzi hao na kuwafunga kamba
miguu na mikono yao huku wakiwaziba midomo yao kwa nguo na kuweka plasta kwenye
vinywa vyao pamoja na pua mazingira yaliyopelekea kushindwa kupumua kwa mlinzi
huyo mzee na hatimaye kufariki dunia.
Alisema
siku ya tukio katibu wa tawi hilo la Chikundi Amcoss Hassani Simkambi pamoja na
mjumbe wa bodi ya chama hicho Desteria Sellemani waliondoka ofisini hapo majira
ya saa 12:00 jioni baada ya kumaliza zoezi la ugawaji fedha kwa wanachama wao kwa
awamu ya kwanza malipo ya pili huku fedha iliyobaki shilingi milioni 44
wakiiacha kwenye mfuko wa sandarusi nyuma ya sanduku la kuhifadhia fedha
kinyume na utaratibu.
Ollomi
alisema viongozi hao walienda kwa katibu mkuu wa chama hicho Philipo Kambanga
kwa ajili ya kupeleka funguo kama ilivyo kawaida ya siku zote lakini kwa
mshangao katibu huyo aliwaruhusu funguo hizo waondoke nazo ili wawahi kufungua
ofisi siku ya pili asubuhi.
Kwa
mujibu wa kamanda huyo alisema mlinzi Bakari Ibrahimu aliyefanikiwa kujiokoa ndiye
aliyeenda kutoa taarifa usiku huo kwa katibu mkuu wa chama hicho na kwamba mara
baada ya kupokea taarifa hiyo naye alitoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji hicho
Clauda Mande majira ya saa 1138 alfajiri na walifanikiwa kufika eneo la tukio na
kukuta mlango ukiwa umevunjwa huku mlinzi mmoja akiwa ameuawa fedha imeibiwa.
Alisema
polisi walifika kwenye eneo la tukio hilo majra ya saa 3:00 asubuhi na
kufanikiwa kufanya mahojiano na wakazi wa maeneo hayo huku wengi wao wakiwa hawaelewi
na kwamba wameshtushwa na tukio hilo la mauaji ya mlinzi huyo.
Kufuatia
tukio hilo jeshi la polisi mkoa wa Mtwara linawashikila watu wanne kwa
mahojiano zaidi wakiwemo mwenyekiti wa chama cha msingi Chikundi Ismail
Chilumba,katibu mkuu wa chama hicho Philipo Kambanga,katibu wa tawi la Mtunungu
Hassani Simkambi,mjumbe wa bodi Desteria Selemani pamoja na Bakari Ibrahimu
ambaye ni mlinzi aliyenusurika kufa.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD