Loading...

HASSAN KESSY AKACHA SAFARI YA SIMBA SHINYANGA,AIDAI MILIONI TANO...

TANGAZO
Beki wa Simba ameamua kutojumuika na klabu hiyo katika safari yake ya Shinyanga kuifuata Kagera Sugar kwa sababu zifuatazo:-
Anasema kwamba anaidai Simba shilingi milioni 5 zilizobakia kama sehemu ya kununua mkataba wake kutoka Mtibwa Sugar.
Pia kwa mujibu wa mkataba wake alitakiwa apewe nyumba ya kuishi hapa Dar es salaam lakini hajapewa pa kuishi na amekuwa akiishi kwa rafiki yake anayecheza naye Simba, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’
Ameongeza kuwa pia kuwa katika mshahara wake alitakiwa alipwe milioni 1.2 lakini analipwa million 1.1 kwa maana kwamba anakatwa laki 1 bila maelezo.
Kwa sababu hizo, Hassan Kessy ‘Danny Alves’ amesema ameamua kuondoka klabuni, na mazoezi haudhurii na hata kwenda Shinyanga na timu haendi hadi alipwe madai yake.

“Niliahidiwa kulipwa baada ya mechi ya Yanga lakini hadi leo sijalipwa nilkiwauliza napigwa chenga”
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top