Loading...

#Ewe Mfanyabiashara Wa Mji Wa Masasi Kuwa "MJANJA WA KWANZA" Kulipa Kodi,Kwa Maendeleo Ya Halmashauri Yako.



OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MJI WA MASASI.

TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI.

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI ANAWAKUMBUSHA WAFANYABIASHARA WOTE KUWA NA LESENI HAI ZA BIASHARA.

LESENI ZA BIASHARA KWA MWAKA MPYA WA SERIKALI 2016/2017 ZIMEANZA KUTOLEWA TANGU TAREHE 1/07/2016 NA KWAMBA WALE WOTE WATAKAOSHINDWA KULIPA NDANI YA SIKU 21 WATATOZWA FAINI.

KUMBUKA KUENDESHA BIASHARA BILA KUWA NA LESENI HAI NI KINYUME NA SHERIA YA LESENI ZA BIASHARA NA.25 YA MWAKA 1972 NA.3 (1, 2 & 3).

MFANYABIASHARA YEYOTE ATAKAYEBAINIKA KUFANYA BIASHARA KINYUME NA SHERIA HII ATACHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA KAMA ILIVYOAINISHWA KATIKA KIFUNGU NA.10 (1) & (2).

AIDHA,MKURUGENZI WA MJI WA MASASI ANAWAKUMBUSHA WAMILIKI WA NYUMBA ZA KULALA WAGENI (GUEST HOUSE) KUWASILISHA KODI ZAO KATIKA WIKI YA KWANZA YA KILA MWEZI.

MWISHO,WAFANYABIASHARA WOTE WANASISITIZWA KUFUATA MASHARTI YA LESENI,IKIWA NI PAMOJA NA KUWEKA LESENI ZAO SEHEMU ZA WAZI KATIKA MAENEO YAO YA BIASHARA KWANI KUTOFANYA HIVYO NI KWENDA KINYUME NA MATAKWA YA SHERIA YA LESENI KIFUNGU NA. 14 (1).

“EWE MFANYABIASHARA WA MJI WA MASASI KUMBUKA KULIPA KODI NI WAJIBU WAKO KWA MUSTAKBALI WA MJI WAKO.

Clarence Chilumba,
Ofisa Habari Halmashauri ya Mji wa Masasi
Agosti 11, 2016.



#Maofisa Mawasiliano Wa Serikali Nchini Watakiwa Kufanya Kazi Kimkakati Katika Utoaji Wa Taarifa Kwa Wananchi.

 Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China Zhao Qizheng na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Hassan Abbas wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini, leo Jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wakimsikiliza Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China, Zhao Qizheng, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini, Leo Jijini Dar es Salaam


Maafisa Mawasiliano Serikalini wametakiwa kufanya kazi zao kimkakati ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao hasa kwenye kipindi hiki cha Awamu ya Tano.

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara na Taasisi za Serikali Waziri wa zamani wa Habari wa Jamhuri ya watu wa China, Mhe. Zhao Qizheng amesema ni muhimu kwa Serikali kuhakikisha kuwa mawasiliano yote yanalenga kuwainua wananchi wake.

“Msemaji wa Serikali inabidi uwe makini katika kazi zako kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati”, alisema Qizheng.

Akifafanua Mhe. Qizheng amesema kuwa ili Tanzania Iweze kufikia maendeleo ya kweli ni muhimu kujenga mfumo dhabiti wa Mawasiliano ya Serikali kwa Umma.

Katika kutekeleza majukumu yao Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini kama wasemaji ni lazima wawe na uelewa mpana kuhusu masuala yanayohusu sekta wanazosimamia ili kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa wananchi.

Pia aliwataka Wasemaji wa Serikikali kujiandaa kabla ya kujibu hoja mbalimbali za kitaifa na Kimataifa zinazohusu Serikali na wananchi ili kutoa taarifa sahihi kwa Vyombo vya habari.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Hassan Abbas amesema ni dhamira ya Serikali kuwasiliana kimkakati ili kuchochea maendeleo.

“Lengo letu ni Kuhakikisha kuwa tunafanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa mawasiliano ya Serikali na wananchi ili kuwapa fursa ya kutoa mrejesho”alisema Abbas.

Katika kuhakikisha azma hiyo inatumia Abbas amebainisha kuwa kwa sasa Serikali inajipanga kufanya maboresho ya mifumo ya Mawasiliano ya Serikali.

Aidha Mawasiliano ya Serikali katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya Tano yanalenga kubadilisha maisha ya wananchi kutoka hali duni kwenda kwenye hali bora.

Mkutano kati ya Waziri wa Zamani wa Habari wa China na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara na Taasisis za Serikali umelenga kujenga uwezo wa Wasemaji wa Serikali ili waweze kuwasiliana na Wananchi kimkakati.


#MATUKIO MBALIMBALI YALIYOJIRI WAKATI WA MAONESHO YA NANE NANE VIWANJA VYA NGONGO-LINDI.

 MJASILIAMALI anayefuga kuku akitoa maelezo kwa makamu wa Rais mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wakati wa maonesho ya Nane Nane Ngongo manispaa ya Lindi.



 KAMANDA wa polisi mkoa wa Lindi Renatha Mzinga akiangalia bidhaa kwenye banda la maonesho la Halmashauri ya mji ws Masasi wakati wa maonesho ya Nane Nane.
 WANANCHI Waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya wakulima kwenye viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.
MKUU wa mkoa wa Lindi Mheshimiwa Godfrey Zambi akipewa maelezo kutoka kwa Afisa Kilimo wa Halmashauri ya mji wa Masasi Philipo Temba wakati wa maonesho ya Nane Nane 2016.

#WAZIRI NAPE MOSES NNAUYE AIPONGEZA KAMPUNI YA MAGAZETI YA SERIKALI KUSHIRIKI NANE NANE

 WAZIRI Wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Moses Nnauye akipata maelezo kutoka kwa mfanyakazi wa kampuni ya magazeti ya serikali.
 WAZIRI wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiwa kwenye Banda la Kampuni ya magazeti ya serikali kwenye maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ngongo Manispaa ya Mji wa Lindi.
 Baadhi ya Watumishi wa kampuni ya magazeti ya serikali wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mheshimiwa waziri Nape Moses Nnauye.
 WAZIRI Nape Moses Nnauye akisaini Kitabu cha wageni kwenye banda la maonesho ya Nane Nane 2016.
 MKUU wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi (Kushoto), akiagana na waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo mheshimiwa Nape Moses Nnauye.








SERIKALI YAPIGA MARUFUKU UCHOMAJI MOTO MISITU KWA WANANCHI WA MIKOA YA LINDI NA MTWARA.

 MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwahutubia wakulima na wananchi kwa ujumla wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wakulima Kitaifa yaliyofanyika Ngongo Manispaa ya mji wa Lindi.

Na Clarence Chilumba,Lindi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hasani amepiga marufuku uchomaji moto wa misitu katika mikoa ya Lindi na Mtwara lengo likiwa ni utunzaji wa mazingira.

Pia amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri katika mikoa hiyo kuhakikisha wanawasimamia wananchi wao katika kuachana na vitendo vya uchomaji wa misitu.
Marufuku hiyo ameitoa leo kwenye kilele cha siku ya wakulima (NANE NANE) kwenye viwanja vya Ngongo Manispaa ya Mji wa Lindi.


 Mbunge wa jimbo la Mtwara Vijijini Mheshimiwa Hawa Ghasia (Kulia) akicheza ngoma na kikundi cha Ngoma wakati wa maadhimisho ya siku ya wakulima.
 MAKAMU wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti es Halmashauri ya Mji wa Masasi Mheshimiwa Sospeter Nachunga kwenye maonesho ya Nane Nane kitaifa 2016.
 WAZIRI wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Charles Tizeba akizungumza na wananchi wa Mikoa ya Lindi na Mtwara Kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wakulima kitaifa yaliyofanyika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.
 WANANNCHI wakisikiliza kwa makini Hotuba Mbalimbali za Viongozi katika maadhimisho ya siku ya wakulima.
WAZIRI wa Fedha Dk.Philip Mpango akiongea na wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara.

#Kama Hauko Ngongo Lindi,Usiangaike Nimekuwekea Matukio ktk picha ya Maonesho ya Nane Nane.

WAZIRI Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa George Simbachawene akipata maelekezo kwenye moja ya Banda la maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Ngongo manispaa ya Mji wa Lindi.

WAZIRI george Simbachawene akiwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego pamoja na Mkuu wa wilaya ya Newala.

Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene akionesha mkoba aliopewa kwenye banda la mfuko wa Afya ya Jamii (NHIF) Kwenye banda lao la maonesho ya Nane Nane.

Waziri wa TAMISEMI akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la maonesho la Halmashauri ya wilaya ya Lindi.

MKULIMA wa Mihogo kutoka kijiji cha Mtama mkoani Lindi Rashid Chilumba akionesha bidhaa zake kwenye maonesho ya Nane Nane.

WATAALAMU wa TANESCO wakitoa Elimu kwa Vitendo namna ya Kumuokoa mtu alioyepatwa na tatizo la Umeme.

Banda la kuku la maonesho ya Nane Nane likiwa kwenye viwanja vya Ngongo manispaa ya Lindi.

 Afisa Habari na Uhusiano wa Halmashauri ya Mji wa Masasi Bwana Clarence Chilumba,(Kulia) akitoa maelezo mafupi ya ukaribisho kwenye Banda la Maonesho la Halmashauri ya Mji wa Masasi kwa mkuu wa mkoa wa Lindi Mheshimiwa Godfrey Zambi alipotembelea banda hilo la maonesho.



 MKUU wa mkoa wa Lindi akiwa ndani ya Banda la Halmashauri ya Mji wa Masasi akikagua bidhaa mbalimbali zilizopo kwenye banda hilo.
Mheshimiwa Godfrey Zambi akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wajasiliamali kwenye banda la maonesho ya Nane Nane Halmashauri ya mji wa Masasi.
MKUU wa mkoa wa Lindi Mheshimiwa Godfrey Zambi akikagua bidhaa kwenye banda la maonesho ya Nane Nane Halmashauri ya mji wa Masasi.
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top